January 27, 2018

MNEC TAIFA SALIM ASAS ASHUSHA NEEMA UWT IRINGA VIJIJINI

Mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha Mapinduzi Salim Asas anayewakilisha Mkoa wa Iringa akionyesha kablasha lenye mipango kazi ya UWT wilaya ya Iringa vijijini Leo baada ya kufungua baraza kuu la UWT 
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijijini Costandino Kiwere akimvisha vazi la heshima mjumbe wa NEC taifa Salim Asas 
Mjumbe wa NEC Taifa salim Asas akivishwa vazi la heshima ya kichifu 
Salim Abri Asas akivishwa vazi la kichifu.sasa anaitwa mwa Abri Mtatifikolo
Salim Asas akifungua baraza kuu la UWT Iringa vijijini Leo
Mwenyekiti wa UWT Iringa vijini akimkabidhi MNEC mpango kazi wa UWT 

............................

MJUMBE wa halmashauri kuu ya CCM Taifa anayewakilisha Mkoa wa Iringa Salim Asas ameahidi kuichangia jumuiya ya wanawake wa chama cha mapinduzi ( UWT) wilaya ya Iringa vijijini kiasi cha shilingi milioni 5 kila mwaka .

Asas ametoa ahadi hiyo Leo wakati akifungua kikao cha baraza kuu la UWT Wilaya ya Iringa vijijini kwenye ukumbi wa siasa in kilimo mjini hapa.

Alisema kuwa lengo la kusaidia jumuiya hiyo no kuitaka ijitegemee pia kuwa na miradi take.


Kwani alisema ameona ni vema kuiwezesha jumuiya hiyo kupata ndoano kuliko kuipa samaki na kuwa kwa kipindi chake chote cha miaka mitano atakayokuwepo madarakani kila mwaka ataichangia jumuiya hiyo kiasi cha shilingi milioni 5 na kwa miaka yote mitano ni sawa na milioni 25.

"Ahadi yangu nitapaswa kuiweka katika maandishi ili familia yangu ijue pale nitakapo tangulia mbele za Haki ahadi hii iweze kutekelezwa na familia maana hatujui la kesho"

Hats hivyo alipongeza jitihada za UWT Iringa vijijini kwa kuwa na mipango ya kimaendeleo kwa jamii tofauti na vyama vya upinzani ambavyo mipango yao ni maandamano na vurugu.

Usikose kusoma gazeti la RAI undani wa habari hii au tembelea Chanel yetu ya YouTube: matukiodaima 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE