January 15, 2018

MMOJA AUAWA NCHINI SENEGAL

Senegal
Jeshi nchini Senegal limearifu kuwa mtu mmoja ameuawa katika mapigano kati ya askari na kikundi chenye silaha katika kanda ya kusini mwa Casamance.
Makabiliano hayo yalifanyika karibu na msitu ambapo watu kumi na wanne waliuawa na washambuliaji wasiojulikana Jumamosi.Watuhumiwa ishirini na mmoja wamekamatwa, akiwemo mmoja nayetuhumiwa kujihusisha na ikiwa ni pamoja na msaidizi mmoja anayehusika wa kundi la wanasiasa wa zamani .
Mkoa huo umeathirika kwa namna moja ama nyingine kutokana na makabiliano hayo yasiyokuwa na tija baina ya serikali na vikundi bya waasi ambao unachochewa na wanasiasa hao wa zamani ili kujitangazia uhuru.
Katika siku za hivi karibuni, Senegal imetuma askari wa ziada na kuanzisha mashambulizi kwa njia ya anga.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE