January 28, 2018

Menyekiti wa maswala ya fedha wa chama cha Republican tajiri Steve Wynn, ajiuzulu

        Steve Wynn ni tajiri mkubwa wa biashara ya mchezo wa kamari                                     Steve Wynn ni tajiri mkubwa wa biashara ya mchezo wa kamari                

Mchangishaji mkuu wa fedha za kisiasa wa chama tawala cha Republican, nchini Marekani, amejiuzulu wadhifa wake kwa sababu ya madai ya kuhusika na makosa kadhaa ya bughdha za ngono.
Steve Wynn, bilionea mmoja mmiliki wa jumba la kuchezea kamari na rafiki mkubwa wa Rais Donald Trump, ametuhumiwa kwa kuhusika katika matendo kadhaa ya bughdha za kingono, dhidi ya wafanyikazi kadhaa wa kike.
Kwa mjibu wa jarida la Wall Street, Wynn -- ambaye aliachia nafasi kama mwenyekiti wa kamati kuu ya kitaifa ya Chama cha Republican maswala ya kifedh-- wakati mmoja amewahi kumlipa mpambaji wake wa makucha mamilioni kadhaa ya dola, ili kuzima madai ya kumbughudhi kimapenzi mwanadada huyo.
Steve Wynn na mkewe wa pili, Andrea Hissom, wakati wa kuapishwa kwa Rais Trump Wynn na mkewe wa pili, Andrea Hissom, wakati wa kuapishwa kwa Rais Trump                
Amepuuzilia mbali madai hayo na kusema hayana msingi wowote.
Anasema, mkewe wa zamani ambaye wangali wakizozana baada ya kutalikiana, ndiye aliyeanzisha uzushi na uvumi huo dhidi yake.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE