January 22, 2018

MBUNGE NEEMA MGAYA ALIVYOPANIA KULETA MAENDELEO MKOA WA NJOMBE

Mbunge   wa viti maalum mkoa  wa  Njombe Neema Mgaya (CCM)

mbunge wa  viti maalum  mkoa  wa  Njombe Neema  Mgaya (CCM) kushoto akikabidhi  vitabu kwa  afisa  elimu wilaya ya  Ludewa Maternus Ndumbaro  kwa  ajili ya  shule  za sekondari  za  serikali na  za  dini
 
mbunge wa  viti maalum  mkoa  wa  Njombe Neema  Mgaya (CCM) kulia  akiwa na naibu  waziri  wa nchi  ofisi ya Rais tawala  za  mkloa naserikali  za  mitaa(TAMISEMI) Josephath Kandege mara  baada ya  kukabidhi vyerehani 370 kwa  wanawake mkoani  Njombe
.............................................................................................................................
Na Francis Godwin-MatukiodaimaBlog
PAMOJA  na  kuwa  kila  serikali  imefanya kazi  ya  kuwaletea  maendeleo wananchi  wake kwa  wakati  wake na  kila  Rais kwa  awamu  yake  amepata  kutekeleza  vema  Ilani ya  chama  cha mapinduzi  (CCM)  binafsi  utendaji   kazi  wa  Rais  Dkt  John  Magufuli umenivutia sana nami  nipo bega  kwa  bega  kuona  mkoa  wanguNjombe   kupata matokeo Chanya.
 “Mimi  Neema  Mgaya  ni moja wa wanawake wabunge  wa  viti maalum ninayetoka  mkoa  wa  Njombe nitaendelea  kuona  siwi mwanamke nisiyetumikia  vema nafasi yangu ya ubunge  huu wa viti maalum  kupitia  CCM.”

“Ninachojivunia serikali   hii ya awamu ya tano ya Rais Dkt Magufuli kwanza imejikita zaidi ktk kuwatumikia wananch
i na hasa kwa maslai ya watanzania wa  kawaida na imeweka rasilimali za Taifa chini ya wananchi wa kawaida kwamba kila mmoja afaidi matunda ya rasilimali za Taifa”.

Mbunge  Mgaya  anasema  katika  CCM  sasa kimeingia kwenye msingi ambayo tangu mwanzo wake kilitakiwa kuwa namna hiyo tulianza kuacha misingi ya chama tukaanza kuthamini watu wenye fedha , wenye fedha walianza kuwa na sauti kubwa ndani ya chama lakini leo hii chama kina sauti juu ya wanachama wake badala ya watu kuwa na sauti juu ya chama nampongeza sana  Rais Dkt Pombe Magufuli  kwa  hili ameweza.

“Tukija katika swala la maendeleo ndani ya muda mfupi wa miaka miwili hii ambayo imepita tumeona maendeleo makubwa yamesukumwa tumeona swala la Elimu bila malipo , miradi ya maji , afya  hata  kwenye swala la utawala sasa hivi watu wanawajibika zaidi,swala la rushwa limezidi kupungua ndani ya muda mfupi tumeweza kuona mambo makubwa yameweza kufanyika”

Anasema  kuwa hatua   ya Rais ya kutaka kulipa madeni ya ndani hatua  hiyo  ni njema  sana kwa  sababu biashara za wananchi wa Tanzania zitaenda kuimarika na  mtaani  pesa  itamwagika  Rais kweli anathibitisha ndani ya mioyo ya watanzania anachokisema ndio anachotenda na anakisimamia yeye mwenyewe.

Kuwa  serikali ya awamu ya  tano kwanza imejikita zaidi katika  kuwatumikia wananchi na hasa kwa maslai ya watanzania wa kawaida na imeweka rasilimali za Taifa chini ya wananchi wa kawaida kwamba kila mmoja ana faidi matunda ya rasilimali za Taifa.

“Rais wetu  kweli anathibitisha ndani ya mioyo ya watanzania anachokisema ndio anachokotenda na anakisimamia yeye  mwenyewe ni Rais wa aina yake kwakweli.

Kweli  binafasi  najivunia sana kuwa na  Rais  kama  huyu  ila  kuendelea  kumuunga  mkono mimi  nikiwa  mbunge  mwanamke  na  mmoja kati ya  wanawake  wenye malengo  ya  kuja  kuwa mwanasiasa  bora  mwenye  kujali  watu kama  Rais Dkt  Magufuli.

“Nimeanza siasa tangu mwaka 2006 nikiwa nafanya masters degree ( shahada ya uzamili) mzumbe chuo kikuu Morogoro nakuendelea na siasa baada ya kumaliza masomo yangu , siasa zangu kwa kipindi cha miaka 7 nimezifanyia wilaya ya kinondoni Dar es salaam na baada ya kupata ubunge kupitia kundi la Vijana kutoka mkoa wa Dar es  salaam baada ya kumaliza kuwatumikia nilihamishia siasa zangu nyumbani kwetu kwenye asili yangu mkoa wa Njombe, hadi  sasa nipo mkoa wa Njombe  nikiwa  mbunge  wa  viti maalum “

Ndoto yangu kisiasa nije kuwa mwanasiasa mkubwa   nitakae  kutendea  haki  chama  change na   serikali  kwa  nafasi  yangu kama  ambavyo  navyofanya  sasa .

Malengo yangu kwa jamii ya Njombe nikuhakikisha kwamba zile changamoto zote zinazozikabili wananchi wa mkoa wa Njombe nashiriki kikamilifu kuzitatua, nakuleta maendeleo katika  jamii yangu ya mkoa wa Njombe .


 

Kazi ambazo  najivunia  na  nimezifanya   kipindi cha miaka miwili 2016/17 baada tu ya kuchaguliwa na  kuapishwa  kuwa mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe  ni pamoja na msaada wa mradi wa vyerehani 370 vyenye thamani zaidi ya mil 90 kwa kinamama wa mkoa wa Njombe ili kuanzisha viwanda vidogodogo kuelekea  Tanzania  ya uchumi  wa  viwanda.

“Lengo la  kutoa  vyerehani  hivi  ni  kuona  wanawake wanajikwamue kiuchumi huku nikiunga  mkono kwa  vitendo juhudi za Mhe. Rais na Serikali kuhimiza uchumi wa viwanda na kuwataka Watanzania kufanyakazi kwa bidii”

Pia  nimetoa msaada wa vitabu vya masomo ya ziada shule 105 za sekondari za serikali, shule za wazazi na za kidini ndani ya mkoa wa Njombe, vitabu hivyo ni vya masomo ya ziada vya Chemistry, Biology,Physics, Mathematics, Geography na literature.

Mbunge Mgaya  anasema  pia  amechangia mifuko ya saruji pamoja na bati katika ujenzi vituko vya afya,ofisi za serikali,shule mbali mbali pamoja na mabweni zikiwemo Shule ya sekondari ya Philipo Mangula tani  moja  ya  saruji ,shule ya sekondari Sovi tani   pia tani  moja ya  saruji .

Maeneo  mengine  ni  ofisi ya serikali kijiji cha Malangali bati 20,ofisi ya serikali ya kijiji uhenga mifuko ya saruji  kituo cha afya cha kijiji cha Dulamu tani moja ya saruji na bati  10,-ujenzi wa bweni la Wanike sekondari bati 10 pamoja na ujenzi wa ofisi ya ccm mkoa Njombe milioni saba    saba .
Anasema  changamoto  kubwa ambayo  wabunge  wa  viti maalum  nchini  wanaipata  akiwemo  yeye  ni kukosa  pesa  ya  mfuko  wa jimbo au  mkoa maana  wao  majimbo  yote  ya  mkoa lazima  wayafikie  ila  hakuna  pesa zinazotengwa  kwa  ajili ya  mfuko  wa  wabunge wa viti maalumu.

“Kila ninachochangia jamii ni pesa inayotokana na mshahara wangu na isitoshe mbunge wa viti maalum jimbo lake ni mkoa mzima kwa maana ya majimbo yote yaliyopo ndani ya mkoa wake mimi  ni  mbunge wa  wote “

Pamoja na  kukosa  pesa  za mfuko  wa  jimbo sitarudi  nyuma  kuendelea  kuwatumikia  wananchi  wa  majimbo  yote pia  kuona  wanawake  wa mkoa  wa  Njombe wanajikwamua  kiuchumi  kwa  kuendelea  kuwawezesha   .

Anasema  Mwanamke  ni  kichwa  cha  familia hivyo  iwapo atawezeshwa  ni  wazi jamii  nzima itafanikiwa  kupitia mwanamke  aliyewezeshwa .

“ Ubunge  wangu  umetokana na  wanawake  wa  mkoa  wa  Njombe  hivyo kidogo  ninachokipata  nitaendelea   kuwakumbuka  ila  rai  yangu  kwa  wale  ambao  wawezeshwa  nao  kuzidi  kuwavuta  wenzao  ili  kunufaika  na uwezeshwaji  huo “

Mgaya  anasema  anapata  ushirikiano  mkubwa  kutoka kwa  wanawake  wa  mkoa  wa  Njombe jamii nzima  pamoja na viongozi  wa  serikali ambao  pindi anapohitaji  kufanya  jambo  kwa  ajili ya  wana Njombe wamekuwa  bega kwa  bega  kuona  wanashirikiana .

Maria Haule  anasema ni mkazi  wa  Ludewa  ambae ni  mmoja kati ya  wanufaika  wa vyerehani anasema  kazi  inayofanywa na mbunge  huyo ni  kubwa  na hakuna  mbunge wa  viti maalum  ambae amefanya  kazi kubwa kama  hiyo ambayo  imekuwa  ikifanywa na  wabunge wa majimbo pekee .
 
Kazi  nzuri  hii inayofanywa na  mbunge  huyo  mwanamke  ni  kielelezo  tosha  kuwa  wanawake wanaweza hata  bila  kuwezeshwa suala  ni  kupewa  nafasi zaidi .
 
Pamoja  na  kazi  nzuri inayofanywa na mbunge  huyu wa  viti maalum bado  kuna haja ya  wabunge  wengine  wa viti maalum kuiga mfano  huu  wa  kuwatumikia  wananchi  kwa  nafasi  walizoomba 
Serikali ya  Tanzania ni  miongoni mwa  serikali inayopenda  kuona  uwiano  wa  uongozi  katika  nafasi  za  uongozi   una  kuwa  sawa .

Tayari   bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  lilifanya marekebisho ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1995 na ya mwaka 2005 yalifanywa na kuongeza idadi ya viti maalum kwa wanawake vilivyoongezwa hadi kufikia asilimia 30.
 
 Katika kuhakikisha kuwa wanawake wanajengewa uwezo wa kisheria na kupata haki zao, sheria kadhaa zimetungwa na nyingine kufanyiwa marekebisho ikiwemo Sheria ya makosa ya Kujamiiana yaani (SOSPA) ya  mwaka 1998, ambayo imefanyiwa marekebisho  na kuhuishwa kwenye Sheria ya Kanuni za Adhabu.
 
         Mwandishi  anapatikana  kwa  simu 0754 026 299
TAZAMA  VIDEO  ZA  MATUKIO  MBALI  MBALI  YA  MBUNGE  NEEMA MGAYA HAPA CHINI
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE