January 21, 2018

MBUNGE DEOGRATIUS NGALAWA NA MWANGA WA MAENDELEO JIMBO LA LUDEWA


                                  Mbunge  wa  Ludewa Deogratius Ngalawa
.................................................................................................................................................
MBUNGE wa  chama  cha mapinduzi (CCM)  jimbo la  Ludewa  mkoani  Njombe  Deogratius  Ngalawa  ni  mmoja  kati  ya  wabunge   waliojipambanua wazi  kwa  wananchi   waliomchagua  kuona wanashuhudia  mwanga   sahihi  wa  maendeleo  kupitia  miradi  mikubwa ya ya  liganga  na  mchuchuma.

Anaandika Mwandishi  wa mtandao  huu Francis Godwin toka  Njombe, kuwa Ngalawa  ambae  hiki  ni  kipindi  chake  cha kwanza cha ubunge  wake anasema  kuwa kasi  kubwa ya maendeleo  ya  wilaya ya  Ludewa itaonekana  zaidi  baada ya  kuboreshwa  kwa miundo  mbinu  hasa barabara  na  tayari  serikali ya  awamu ya  tano  chini ya  Rais Dkt  John Magufuli  imekuwa bega  kwa  began a wananchi  wa Ludewa  kuona barabara  ya Njombe- Ludewa  inajengwa  kwa  kiwango  cha  lami.

Akijibu  maswali ya  wananchi  kupitia  kundi la WhatsApp la  jimbo  kwa  jimbo Tanzania  mbunge  Ngalawa  alisema  kuwa ni  ukweli  usiopingika   kuwa  wilaya  ya  Ludewa ni moja kati ya  wilaya  zenye  utajiri  mkubwa  ila  ni  vigumu  utajiri   huo  kuweza  kuanza  kuwanufaisha   wana Ludewa  na  watanzania   iwapo  miundo  mbinu haitaboreshwa .

“ Ni  kweli  jimbo la  Ludewa ni  tajiri  ila  kilichokosekana  ilikuwa ni  mitazamo sahihi  mfano uanzishwaji  wa  miradi ya  Liganga  na mchuchuma   huwezi   sema  itaanza  kabla ya   kuwekwa  miundo  mbinu bora ndio mimi kama  mbunge  nimejikita  katika  barabara  zinazoelekea  katika  miradi  hiyo  kipaumbele  kingine ni umeme ambao  kwa  sasa  kupitia  mradi  wa  umeme  vijijini (REA)  umeme  umeendelea  kusambazwa  vijijini pia  jitihada za  maji  nazo  zinaendelea  kufanyika lengo kuona wananchi  wanapatiwa   huduma  ya maji “

Anasema  kuwa amekuwa mbele  kuwapigania  wananchi  wake  bungeni  na  serikali  imekuwa  sikivu na  kuwa  kilimo  cha  umwagiliaji  bonde  la Lifua ,Mkiu na Ruhuhu na  kuwa  iwapo  miradi ya  Liganga na  mchuchuma  ikianza  wakati  wananchi  hawajaandaliwa  kiushindani miradi   hiyo  inaweza  kuwafanya  wananchi  kuwa  watumwa  katika  miradi  hiyo  hivyo  mkakati ni  kuona  wananchi  wanaandaliwa  ili  wasiwe  watazamaji katika  miradi  hiyo  mikubwa .

Mbunge Ngalawa  anasema  kuwa  ni  lazima  kuweza  kuwa na  viwanda  vidogo  vidogo  vya  samaki  hasa  vya  kuhifadhi  kwani  bado   watu  wengi hawajawa na  uelewa  kwani  samaki  pekee  za mapambo  hawajanufaika  zao kwa  kuzitafutia  soko .

  Tatizo letu  wanasiasa  tunashindwa  kuwasaidia  wananchi  waliotuchagua kwa  kueleza  ngojera  zaidi majukwaani  badala ya  namna ya  kuwaelimisha  kubaini  fursa na  kuzifanyia  kazi kwa  mfano  Miradi  hiyo  itawezesha  wananchi  zaidi ya  313,000 kupata  ajira  na  kunufaika na  fursa  za  miradi  hiyo  mikubwa  ya  Liganga na  Mchuchuma”

 

Aidha  anasema  kuwa  sekta ya  Kilimo   kinu  cha  kusindika  unga  kimewasili Mavanga  na ni mkakati  wa kuanzisha  kiwanda  cha  kusaga  unga na  kukoboa  pamoja na  kuweka virutubisho  na  kusindika tani tatu  hadi  tano   kwa  saa jambo  ambalo ni hatua  kubwa kwani  itatengeneza  pia  ajira na  hii ni safari ya  utekelezaji wa azma ya  serikali ya Tanzania ya  viwanda.

Mazao  ya  wakulima  yatanunuliwa  robo ya mahindi  yanayolimwa na  wana Ludewa yatauzwa ndani ya  wilaya katika  taasisi ya  Ludewa  Agribusiness pia  kunaanzishwa  kiwanda   kingine  cha  chakula  cha  mifugo  kwa  kuuza  pumba  inayotokana na  kiwanda  cha  unga  hivyo  chakula  cha mifugo  mbali mbali na  Samaki kwenye  mabwawa ya  wananchi  na   kuongeza ufugaji wa ng’ombe ,Nguruwe  na mifugo  mingine .

Kilimo  cha  Korosho  kumekuwepo na mafanikio  makubwa  kwa  kufanikiwa  ku kuotesha vitalu  vya   miche  ya  korosho 152,000 kwa  mwaka   2016 na  miche  hiyo  ilitolewa  kwa  wananchi  lengo  likiwa ni  kuanzisha  ubanguaji wa  korosho  wenyewe  ili  kuondokana na  ulanguzi  wa  korosho  usio  na faida kwa  mkulima .

Anasema  kuwa  tayari  wameomba  kwa  mwaka  wa  fedha 2018/19 pesa  ya  kuendelea  kuboresha  barabara na  tayari  naibu  waziri wa wizara   husika  amepata kufika  Ludewa  kuona  kazi  hiyo  inaanza  kwa  wakati .

Kuwa  barabara  ya  Njombe- Ludewa  na Manda  usanifu   wa  kina  ulisha anza  June 2016 na  mkataba  wake  ulishasainiwa  toka Agosti 22  mwaka 2016.

Pia  kuna   zoezi la  kuchimba brabara  toka  Lumbila  kwenda Lupila  kwa  sasa tumeanza  kulima  kwa  nguvu za  wananchi  toka Nkanda , kwenda  Lumbila kwa  kulima   Kilometa  7 bado  Kilometa 3  kufika Lumbila , baadae  Chenjale  hadi Kilondo  na  Makonde na  maeneo mengine .

Kuhusu  Afya  anasema  ameendelea  kuchangia  bati  kwa  ajili ya  ujenzi  wa  vituo  vya  afya 15  na  Zahanati 16 katika  jimbo   hilo la  Ludewa .

Wakimpongeza  mbunge  Ngalawa  kwa  kueleza  kazi  kubwa  aliyoifanya  jimboni mwanakundi  Vicky  Ntetema  ambae ni  mmoja kati ya  wanahabari nchini  alisema  kuwa  kazi  ya  mbunge   huyo  imejieleza na  inaonekana  hata kwa  asiye mkazi  wa  Ludewa na  kutaka  wabunge  wengine  kutowa  nyuma  kueleza  shughuli  za  kimaendeleo majimboni .

  Wabunge   wengi  wanapokuwa majukwaani  kuomba  kura  kwa  wananchi wamekuwa na  sura  za  unyenyekevu  pamoja na  kutoa  ahadi  nyingi  ila  baada ya  kuchanguliwa  wengi  wao  wamekuwa  si watekelezaji  wa ahadi  zao na  hata  ule  upole   walioonyesha   wakati  wa  kuomba kura  huwa  hauonekani  tena “

Ntetema  alimtaka  mbunge   huyo  kuweza  kuwaondoa  sintofahamu  kuhusu  ziwa  nyasa  kuwa na  samaki  adimu  duniani  ambao ni  kivutio zaidi na  kujua   jitihada za  eneo  hilo la  Ziwa  Nyasa  kufungua  lango la  utalii.

Akijibu  swali la  Ntetema  mbunge Ngalawa  anasema    wakati  wabunge  wanaomba  kura wamekuwa  wanyenyekevu ila  wakipata  wengi  wao  huwa na majibu ya  ukakasi  kwa  wapiga  kura kuwa  hali  hiyo hutokana na  muuliza  swali  japo  tabia za  wabunge  zimetofautiana  wapo  ambao  muda  wote ni  wanyenyekevu  kwa  wapiga  kura  wake .

Kuhusu  samaki  wa mapambo  kuwa  samaki  hao  wapo  ila  shida ni  miundo  mbinu  na  uwekezaji katika Beach  na  fukwe  za  ziwa   hilo  huku  barabara  inayoelekea  katika fukwe za  ziwa  nyasa   ipo  mbioni  kujengwa  na  waziri  mwenye  dhamana  kafapelekewa  ombi la  ujenzi wa  barabara   hiyo.

 

 kuwa  serikali  ya  wilaya  na  mkoa  inaendelea  kupambana  kuona mazingira  rafiki  ya  fukwe  za  ziwa nyasa  ili  kuvutia utalii   kuboresha  Kilimo , uvuvi, ufugaji na  biashara   mbali mbali kama  sehemu ya  wananchi  kujakutumia  fursa za  miradi  hiyo  itakapoanza .

 Anasema  kuwa  katika  eneo la  uvuvi mkakati  wa  kwanza  ni kuboresha  miundo  mbinu  ya   fukwe za  ziwa  nyasa  pia mifumo  ya kiuvuvi  bado  ni  ya  zamani  japo  elimu  inatolewa  juu ya kulinda  uvuvi  salama na  endelevu  kwa  kulinda  mazalio ya  samaki katika  mito  pamoja na   uundaji  wa  vyombo vya  kuvulia na   packing kabla  haijaenda kwa  mlaji .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE