January 23, 2018

MAKONDA: WATU HAWA NAWAHITAJI OFISINI KWANGU


Mkuu wa Mkuu wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Dar es salaam waliodhulumiwa mali zao ikiwemo viwanja, nyumba, mashamba, magari na vifaa vingine kufika ofisini kwake.
Makonda amewataka watu hao kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ilala Boma kuanzia January 29 hadi February 02 kwaajili ya kupatiwa msada wa kisheria.
Mkuu wa mkoa huyo amefunguka hayo leo na kusema kuwa amewaanda wanasheria magwiji wa kutosha kwaajili ya kusikiliza matatizo na changamoto za wananchi na kudai wananchi wanapaswa kufika na nyaraka na vielelezo halali ili wapatiwe haki zao.
Makonda ameamua kufanya hili baada ya kubaini uwepo wa baadhi ya wananchi wanyonge wanaodhulumiwa mashamba, mali zao na kunyanyasika kwa kuporwa haki zao na watu wenye uwezo kifedha au wanasheria wenye utaalam wanaokandamiza wanyonge.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE