*Asema waache kuwavuruga watumishi, madiwani
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaonya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Bi. Isabella
Chilumba na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk. Oscar Mbyuzi waache
malumbano ambayo yanawavuruga watendaji walio chini yao.
Ametoa
agizo hilo jana (Jumamosi, Januari 6, 2018) wakati akizungumza na
watumishi na madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa kwenye kikao
kilichofanyika hoteli ya Mt. Vicent, mjini Mbamba Bay, wilayani Nyasa
mkoani Ruvuma.
Amesema
katika ziara zake zote za mikoani, amekuwa akipata malalamiko mengi
kwenye Halmashauri na mabaraza ya madiwani lakini katika wilaya ya Nyasa
amekuta hali ni shwari isipokuwa kuna migogoro midogo kwenye uongozi
wa juu.
“Tatizo
ni dogo huku juu, bado mnavurugana Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi. Ninyi
ni viongozi wa juu, acheni kuvurugana, fanyeni kazi. Mkigombana
wanaoumia ni wananchi,” alisema.
“Mkuu
wa Wilaya anaweza kuingia kwenye kikao chochote cha Halmashauri na kudai
apewe taarifa, mpeni. Yeye siyo mjumbe wa kikao hicho lakini anayo
mamlaka ya kushiriki.”
“Mkurugenzi
wewe ni mtendaji mkuu, tumekukabidhi watumishi uwaongoze. Tumekukabidhi
fedha kwa ajili ya maendeleo ya wilaya hii. Mtu akizitamani, mwambie
hizi fedha zina maelekezo rasmi, hazipaswi kwenda kokote,” alisisitiza.
Aliwataka
madiwani wasijenge tabia ya kuongeza siku za vikao kwa makusudi ili tu
wapate posho za ziada. “Msitengeneze siku za ziada na kumpa presha
Mkurugenzi. Kama kikao ni cha siku moja, basi kiishe. Siyo kulaza ajenda
ili mmalizie kesho yake. Mkurugenzi akiwanyima fedha, msianze kugombana
naye kwa sababu yeye hana fedha za kumgawia mtu,” alisisitiza.
AWEKA JIWE LA MSINGI KITUO CHA KUPOZEA UMEME NJIA YA MAKAMBAKO - SONGEA
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameweka jiwe la msingi kwenye mradi wa njia ya
kusafirisha umeme wa kilovoti 220 kutoka Makambako hadi Songea na
kuahidi kuwa Serikali itaendelelea kuwasambazia umeme wananchi wote.
Ametoa
ahadi hiyo leo (Jumapili, Januari 7, 2018) wakati Akizungumza na
wananchi wa eneo la Unangwa nje kidogo ya mji wa Songea, mara bada ya
kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa kituo cha kupozea umeme.
Waziri
Mkuu amesema ujenzi huo unaenda sambamba na ahadi ya Mheshimiwa Rais,
Dk. John Joseph Magufuli ya kuwataka Watanzania wapate umeme kwa
urahisi. “Mheshimiwa Rais ameshusha gharama za umeme kutoka sh. 380,000
hadi sh. 27,000. Zamani ulikuwa unalipia fomu za kuomba umeme, sasa hivi
nazo amesema zitolewe bure. Nguzo za umeme zilikuwa zinatozwa sh.
150,000, sasa hivi amesema zitolewe bure,” alisema.
Waziri
Mkuu amesema zamani mikoa ya Njombe, Iringa, Ruvuma, Songwe, Mtwara na
Lindi ilikuwa na matatizo sufu ya kupata umeme lakini hivi sasa mikoa ya
Mbeya na Iringa imepata suluhisho baada ya kukamilika kwa mradi wa
umeme wa kilovoti 400 wa kutoka Iringa hadi Shinyanga.
“Sasa hivi tunaingia Njombe na Ruvuma na baadaye tutaenda Mtwara na Lindi,” alisema.
Alitumia
fursa hiyo kuwaomba wakazi wanaoishi jirani na mahali kituo hicho
kinapojengwa, wawe walinzi wakuu wa mali za mkandarasi ili mradi huo
uweze kukamilika mapema. “Eneo hili lina saruji, nyanya na nondo, si
vema watu wachache wjiokeze na kuiba vifaa vya ujenzi. Saidieni kulinda
eneo hili, na mali za mkandarasi ili mradi ukamilike kwa wakati,”
alisisitiza.
Akitoa
taarifa ya ujenzi wa mradi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Dk. Titus Mwinuka alisema mradi huo utakapokamilika utaunganisha vijiji 120 na wateja 22,700.
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa ofisi za
TANESCO mjini Songea ambalo litagharimu sh. bilioni 2.27. Ujenzi wa
jengo hilo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Machi, 2018.
Akimkaribisha
kuzungumza na watumishi wa TANESCO na wananchi waliohudhuria hafla
hiyo, Waziri wa Madini, Dk. Medard Kalemani alisema jengo hilo ni moja
ya majengo makubwa saba nchini ambayo yatakuwa makao makuu ya kimkoa ya
TANESCO.
Majengo
mengine yatajengwa kwenye mikoa ya Singida, Kilimanjaro, Mtwara,
Njombe, Pwani, Geita na Kigoma. “Kukamilika kwa ofisi hizi haimaanishi
wafanyakazi wakae ofisini na kufaidi viyoyozi. Ni lazima waende nje
kuwafuata wateja,” alisisitiza.
Dk.
Kalemani alisema chini ya mradi wa kusafirisha umeme wa kilovoti 220
kutoka Makambako hadi Songea, Serikali imeamua kujenga vituo vya kupozea
umeme huko Makambako, Madaba na Songea ambavyo vitakamilika Agosti 30,
2018.
“Kukamilika
kwa mradi huo kutaiepusha TANESCO na mzigo mkubwa wa kutumia fedha
nyingi kununua mafuta mazito ambao pia utapunguza gharama za umeme kwa
watumiaji. Kabla ya hapa, TANESCO ilikuwa inatumia sh. milioni 900 kwa
siku kugharimia mafuta hayo,” alisema.
Mapema, akitoa
taarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa TANESCO,
Dk. Titus Mwinuka alisema ujenzi wa jengo hilo ambao umefikia asilimia
78, unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 31, mwaka huu.
“Gharama
za ujenzi kwa jengo zima ni sh. bilioni 2.198 na gharama za mshauri ni
sh. milioni 78 na gharama zote zinafikia sh. bilioni 2.276. Fedha hizi
zimetolewa na Serikali,” alisema.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Madiwani na Watumishi wa Halmashauri
ya Nyasa, katika Hoteli ya Mt. Vicent iliyopo Mbambabay, Mkoani Ruvuma,
Januari 6, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiongea na Madiwani na Watumishi wa Halmashauri
ya Nyasa, katika Hoteli ya Mt. Vicent iliyopo Mbambabay, Mkoani Ruvuma,
Januari 6, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya Nyasa, eneo la Kilosa Bambabay katika Wilaya ya Nyasa, Mkoani
Ruvuma, Januari 6, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati akifungua Bwalo la Chakula
katika Shule ya Sekondari Bambabay, Wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma,
Januari 6, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ngoma ya mganda,katika Tamasha la
utalii lililofanyika Bambabay, Wilaya ya Nyasa, Mkoani Ruvuma, Januari
6, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi, kutoka kwa Bibi Cecilia Manyai,
katika Tamasha la utalii lililofanyika Bambabay, Wilaya ya Nyasa, Mkoani
Ruvuma, akiwa ni Mgeni rasmi katika Tamasha hilo, Januari 6, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi, kutoka kwa Mzee Gidion Ndembeka,
katika Tamasha la utalii lililofanyika Bambabay, Wilaya ya Nyasa,
Mkoani Ruvuma, akiwa ni Mgeni rasmi katika Tamasha hilo
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea zawadi ya ungo, kutoka kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella
Manyanya, katika Tamasha la utalii lililofanyika Bambabay, Wilaya ya
Nyasa, Mkoani Ruvuma, akiwa ni Mgeni rasmi katika Tamasha hilo, Januari
6, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 comments:
Post a Comment
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE