January 3, 2018

MADIWANI WA CHADEMA IRINGA MJINI WAJIUZULU PICHA ZA MBUNGE WAO ZAVUJA AKILA MAISHA

mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akichoma nyama picha zilizoenea mitandaoni Léo wakati madiwani wake wakijiuzulu 
Mstahiki meya Chadema Iringa mjini akiwa katika maandalizi ya kusubiri nyama choma 
Diwani wa Mtwivila kupitia Chadema akiperuzi 
Nyama choma ya mbunge Msigwa 
Aliyekuwa Diwani wa Kwakilosa Joseph Lyata aliyejiuzulu leo 

Picha za mbunge wa jimbo la Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa akiwa anachoma nyama na madiwani baadhi wa Chadema mjini Iringa zazua ngunzo mitandaoni leo. 

Wengi wahoji sababu ya mbunge huyu kujichimbia na baadhi ya madiwani na kushindwa kula na yatima jimboni mwake Kuwa kitendo hicho hawajapendezwa nacho. 

Baadhi ya madiwani wa Chadema ambao waliomba kutotajwa mtandaoni wamesema kuyumba kwa chama kunatokana na ubinafsi wa baadhi ya viongozi wa chama hicho. 

Huku aliyekuwa Diwani wa kata ya Kihesa Edga Mgimwa akidai kuwa kazi imeanza ila mbunge aendelee kula nyama choma huku akitambua kazi ya halmashauri kurudi CCM imeanza. 

Kwa sasa Chadema ina  kata saba ambazo ni Mwangata, Isakalilo, Ilala , Mtwivila, Gangilonga, Mkwawa na Mvinjeni ambazo Chadema wamebaki nazo kati ya kata 14 za jimbo la Iringa mjini. 

CCM ilikuwa na kata sita  pekee ambazo ni Mshindo, Mlandege, Kitanzini ,Kitwiru na Nduli na sasa Kihesa ambayo diwani wake alipita bila kupingwa. 

Hivyo iwapo chadema watasusia uchaguzi  Tena wa kata hizi mbili ya Kwakilosa na Ruaha ni wazi Chadema itabaki na kata 7 huku CCM ikiwa na kata nane hivyo kuwazidi chadema kata moja. 

CCM ina wabunge wawili wa viti Mwalimu wanaoingia katika baraza la madiwani na kufanya idadi yao kufikia 10 na Chadema ina wabunge wawili mbunge wa jimbo na viti maalumu ambao idadi yao inafikia 10.

Ila pia Chadema kwa sasa ukiacha madiwani wawili waliojiuzulu wale wa viti maalumu ilikuwa na madiwani sita sasa imebaki na madiwani wanne ila iwapo wataapishwa hao wawili itakuwa na madiwani wa viti maalumu sita na CCM ina diwani mmoja wa viti Mwalimu. 

Hivyo ni wazi Chadema itakuwa na madiwani 16 na CCM itakuwa na madiwani halali 11 hivyo ili halmashauri kufanywa uchaguzi upya na CCM kuchukua halmashauri lazima CCM iwe na wajumbe halali wa baraza la madiwani watakao piga kura japo 17 .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE