January 12, 2018

KASI HII YA MADIWANI CHADEMA KUENDELEA KUJIUZULU NI SAFARI YA MBUNGE MSIGWA KUPOKONYWA HALMASHAURI KABLA YA MWAKA 2020

Mbunge wa  Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akiwa ofisini kwake
madiwani  waliojiuzulu kutoka  Chadema ,Edga Mgimwa kulia,Oscar Kafuka (mkwawa) na Baraka Kimata (Kitwiru). ...........................................................................................................................
KASI  hii ya  kujiuzulu kwa  madiwani  wa  chama  cha  Demokrasia na maendeleo (Chadema) jimbo la  Iringa mjini  si safari nzuri kwa  mbunge wa   jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Peter  Msigwa (chadema)  hii ni safari ya Chadema kupoteza Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa kabla ya mwaka 2020 kufika .
Kuongezeka kujiuzulu kwa diwani wa Mkwawa Oscar Kafuka  kumeongeza idadi zaidi ya wimbi la madiwani wa Chadema  kujiuzulu na  hivyo kama msimamo  wa  Chadema ukawa ule wa kutoshiriki uchaguzi  basi ni wazi CCM itakuwa na kata 10 kama watashinda  zote na Chadema  kubaki na kata 8 pekee .

Ni  wazi  chama chochote  cha  siasa kina mipango na  mikati yake  kama  ilivyo kwa  wabunge ,madiwani na hata  Rais kuona kuwa alichopanga  kinatimia iwe katika  maendeleo ama katika  siasa hivyo si  rahisi  kuunga  mkono  familia  yako kusambaratika .

Ifahamike kuwa kila  diwani  ama  mwanachama anayetoka Chadema na  kujiuzulu Iringa mjini wanamtaja mbunge  mchungaji  wangu Msigwa kuwa anahusika kuondoka  kwao  na mara  zote Msigwa amekuwa akiweka  wazi kuwa wananunuliwa na wote  waondoke abaki  peke yake si kauli nzuli  kusema  wananunuliwa kwa uelewa wangu anayenunuliwa ni aliyesokoni hivyo  Chadema  Iringa  mjini jiulizeni kwanini  wapo  sokoni hao ?

Siamini katika sababu baadhi  walizozitoa  juu ya  mwenendo  wa Chadema  Iringa  ila naamini moja tu ya ubabe  kuwa mbunge  hili ndilo anguko la  chadema  Iringa  mjini .

Mbali ya  ubunge na uenyekiti  wa kanda ya Nyasa mbunge  Msigwa lazima  ajitafakari upya  wakazi  wa jimbo la Iringa walimuamini na hata kumpa ubunge na  kuwatosa  CCM pia  viongozi  wa Chadema kanda ya  Nyasa walimpa imani  kubwa ila  heshima  hii ni  bure  iwapo hajitafakari na  kujenga  Chadema ama  waliomuamini .

Hebu tutazame  idadi  hii ya   madiwani    chama  cha  Demokrasia na  maendeleo  (chadema)  jimbo la  Iringa  mjini  kujiuzulu   inayozidi    kuongezeka   na  kufikia madiwani nane  sasa ni ya  kujivunia  kuwa unajenga  chama ama  unabomoa ?

Joseph Lyata diwani  wa Kwakilosa aliyejiuzulu   amesema  kuwa  kujiuzulu  kwake  kumetokana na mahusiano mabaya  ya  kufifisha maendeleo kati  yake na  viongozi wa  juu wa Chadema  hicho akiwemo  mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji  Peter  Msigwa  ambae  ni  mbunge wa   jimbo  la  Iringa mjini pamoja  na  uongozi wa juu wa Chadema  ukiongozwa na mwenyekiti  wake  Taifa Freeman  Mbowe.

Lyata  alisema  kuwa  mara kwa mara  amekuwa  akiandika  barua  kwa  uongozi wa  juu wa Chadema  Taifa   kuelezea  malalamiko yake ya  mahusiano mabaya kati yake na  mbunge wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Msigwa  ila wamekuwa  wakipuuza na  kuwa hajaona  sababu ya  kuendelea  kubaki ndani ya  chama  hicho  japo  safari yake ya  siasa  itaendelea  kupitia  chama  chochote ikiwezekana  hata  CCM .

"  Vyama  vya  siasa  vipo  vingi  kuna  CUF , ACT  Wazalendo  na  CCM  hivyo  nitachagua  ni  chama gani  kitanifaa  kufanya  siasa  zangu ila  hata  CCM nipo  tayari  hakuna  ubaya "

Alisema  kuwa figisu  figisu kati  yake  na  mbunge  Mchungaji Msigwa  zilianza toka  akiwa naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa na  hofu ya mbunge  Msigwa  ni baada ya  kuhisi kuwa anautafuta  ubunge wa  jimbo  hilo mwaka  2020 .

"  Mbunge alikwenda katika  chombo kimoja wapo  cha  utangazaji mjini  Iringa (Radio jina limehifadhiwa ) na  kutangaza  kuwa Lyata  anautafuta  ubunge kwa  nguvu na hata  wezi  ila  niwa  wazi  sioni  kosa la  kuzuiwa  kugombea  ubunge  nikitaka na muda  ukifika  nitagombea   ila  namhakikishia  kuwa sijaondoka  katika  Chadema kutokana na kununuliwa nimeondoka  kutokana na mahusiano mabaya  kati yangu na mbunge Mchungaji Msigwa na  wapo  wengi  wanataraji  kuondoka na kujiuzulu nafasi zao  za  udiwani " alisema  Lyata

Kuwa  mchakato  wa  kumpata  naibu  meya  Manispaa ya  Iringa nafasi  ambayo  alikuwa  akiwania  mbunge aliweza  kuingilia mchakato   huo  na  kupanga  mtu  ambae  alimtaka  na  malalamiko  yake  alifikisha  ngazi  za  juu  ila  walikaa  kimya  huku  uongozi wa kanda  kuptia  katibu   wake ulimpuuza kabisa na  kuishia  kusema kuwa ni msaliti .

" Uchaguzi   mdogo wa udiwani Kimala Kilolo na  Kitwiru  mimi na Frank  Nyalusi  hatukupangwa  kushiriki kampeni Kitwiru  kwa  hofu ya  kutujenga  kisiasa  katika mbio za ubunge  tulipangwa Kilolo ila  kata  yangu  imepata maafa  ya nyumba  kuezuliwa  mbunge  hadi  sasa pamoja na kuwa na taarifa  hakuweza  kufika  aliyefika ni mkuu wa mkoa na mkuu wa  wilaya  ambao  waliweza  kunisaidia hadi  kuezeka nyumba   za  wananchi wangu ila mbunge badala ya  kushukuru  ameishia  kunilaumu  kuwa  kwanini nimeezeka nyumba na pesa nimepata wapi "

Hata   hivyo  Lyata  alisema  kwa  ajili ya kuonyesha ana  nguvu ya  kisiasa  kuliko  mbunge Mchungaji Msigwa ataendelea kufanya  siasa  na  kuwa suala la ubunge 2020 asubiri  muda  ufike  ila nyuma  yake  kuna  kundi  kubwa ya madiwani  na  viongozi wa chadema  watakaomfuata bila  kutaja majina  na  idadi yao  alisema  anaungwa mkono  na  madiwani  hao kwa uamuzi  wake .

Kuhusu  tuhuma  za  kununuliwa na  CCM kwa  zaidi ya  milioni 200 Lyata  alisema hajanunuliwa na kama amenunuliwa basi ni  mmoja  mwa  viongozi  wenye  sifa  kuzidi  ya  hao  wanaoeneza uvumi huu maana anayenunuliwa ni  yule anayekubalika na  aliyejiweka  jikoni kama  mmoja kati ya madiwani wa Chadema  ambae amekuwa  akieneza  uvumi ila huku  akitafuta  kununuliwa na  wana CCM

Kwa  upande  wake  Edga  Mgimwa  aliyekuwa  diwani wa  Kihesa  alisema  kuwa amevutiwa na kujiuzulu kwa Lyata  na  kuwa katika mkakati  wake  wa   kufanya kazi kama  kada wa CCM  jimbo la  Iringa ni madiwani  wengi  watajiuzulu .

Mbali ya Lyata na  Mgimwa  madiwani  wengine  waliojiuzulu kwa mwaka  jana na  sasa ni aliyekuwa diwani wa kata ya  Kitwiru  kupitia  Chadema  Baraka  Kimata  ambae  ni diwani  tena wa kata  hiyo  kupitia  CCM , pia  wapo madiwani  wa  viti maalum  wawili Husuna  Ngasi na Leah  Mleleu .

Mapema  mwaka jana akizungumza na  wanahabari mjini hapa  juu ya kujiuzulu kwa madiwani  wanne mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji Msigwa  ambae ni  mbunge  wa  jimbo  hilo  alisema  kuwa kuna  mkakati wa CCM kuendelea  kununua madiwani na  kukanusha malalamiko ya madiwani hao  kuwa yeye  ni  chanzo cha  wao kujiuzulu kwao .

Huku naibu  meya  wa Manispaa ya  Iringa  Dady  Igogo  alisema  kuwa chama  kimewanunulia  vifaa maalum   kwa  ajili ya madiwani wa Chadema wanaonunuliwa  kurekodi mazungumzo  ya  kununuliwa  kwao .

Hii ni  wazi  kuwa Chadema  jimbo la Iringa   Iringa  mjini  kuna  cha  kujifunza kwa viongozi  wake kuwa ubora  wa mtu  si kuongea  ni  kujenga  kwake  idadi  hii imezidi   kuongezeka   na  kufikia madiwani  nane  sasa  baada ya watatu kujiuzulu pamoja na  katibu  wa chadema mkoa  wa Iringa  Oscar Ndale  .

Mbogo  na  Ndale  walisema   kuwa  kujiuzulu  kwao kumetokana na mahusiano mabaya  ya  kufifisha maendeleo  kwenye kata  yake pamoja na mabavu  ya  viongozi w juu wa Chadema .

kati  yake na  viongozi wa  juu wa Chadema  hicho akiwemo  mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji  Peter  Msigwa  ambae  ni  mbunge wa   jimbo  la  Iringa mjini pamoja  na  uongozi wa juu wa Chadema  ukiongozwa na mwenyekiti  wake  Taifa Freeman  Mbowe.

"  Vyama  vya  siasa  vipo  vingi  kuna  CUF , ACT  Wazalendo  na  CCM  hivyo  nitachagua  ni  chama gani  kitanifaa  kufanya  siasa  zangu ila  hata  CCM nipo  tayari  hakuna  ubaya "
Alisema  kuwa  mbunge Msigwa  amekuwa  akimfanyia  diwani  mwenzao Joseph Lyata figisu  figisu toka  akiwa naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa na  hofu ya mbunge  Msigwa  ni baada ya  kuhisi kuwa anautafuta  ubunge wa  jimbo  hilo mwaka  2020 .

Diwani  Mbogo alisema  kwa  sasa atabaki  mwanasiasa   huru  na  iwapo  mbunge  Msigwa na mstahiki meya  Alex Kimbe wataondoka  hata  leo  chadema basi atarejea  Chadema  ila  kama   wataendelea  kubaki hatarudi  kamwe .

Kwa  upande  wake aliyekuwa  katibu  wa Chadema  mkoa ,Ndale  alisema  kuwa kuyumba  kwa chadema  Iringa mjini  kumesababishwa na mbunge   kutokuwa na ushirikiano mzuri  na  wenzake na mara  kadhaa  wamekuwa  wakimuonya ila  bado  anaendelea  na kuwa  Mbowe pia  amesababisha  kujiuzulu kwake  nafasi hiyo  na  kwa  sasa  atajiunga na  CCM .

Ndale  alisema aliomba kujiunga na  CCM na amekubaliwa na  hivyo ataendelea na  Siasa  kupitia CCM huku akisema uhai  wa Chadema  Iringa  mjini  umefika  mwisho .

Kwa  upande  wake Joseph Lyata  aliyekuwa  diwani kata ya  Kwakilosa  alisema siasa ndani ya  Chadema kwake  imemshinda hivyo ameamua  kuondoka  ndani ya  chama  hicho na  kuwa  mwanasiasa  huru .

"  Mbunge alikwenda katika  chombo kimoja wapo  cha  utangazaji mjini  Iringa (Radio jina limehifadhiwa ) na  kutangaza  kuwa Lyata  anautafuta  ubunge kwa  nguvu na hata  wezi  ila  niwa  wazi  sioni  kosa la  kuzuiwa  kugombea  ubunge  nikitaka na muda  ukifika  nitagombea   ila  namhakikishia  kuwa sijaondoka  katika  Chadema kutokana na kununuliwa nimeondoka  kutokana na mahusiano mabaya  kati yangu na mbunge Mchungaji Msigwa na  wapo  wengi  wanataraji  kuondoka na kujiuzulu nafasi zao  za  udiwani " alisema  Lyata

Kuwa  mchakato  wa  kumpata  naibu  meya  Manispaa ya  Iringa nafasi  ambayo  alikuwa  akiwania  mbunge aliweza  kuingilia mchakato   huo  na  kupanga  mtu  ambae  alimtaka  na  malalamiko  yake  alifikisha  ngazi  za  juu  ila  walikaa  kimya  huku  uongozi wa kanda  kuptia  katibu   wake ulimpuuza kabisa na  kuishia  kusema kuwa ni msaliti .

" Uchaguzi   mdogo wa udiwani Kimala Kilolo na  Kitwiru  mimi na Frank  Nyalusi  hatukupangwa  kushiriki kampeni Kitwiru  kwa  hofu ya  kutujenga  kisiasa  katika mbio za ubunge  tulipangwa Kilolo ila  kata  yangu  imepata maafa  ya nyumba  kuezuliwa  mbunge  hadi  sasa pamoja na kuwa na taarifa  hakuweza  kufika  aliyefika ni mkuu wa mkoa na mkuu wa  wilaya  ambao  waliweza  kunisaidia hadi  kuezeka nyumba   za  wananchi wangu ila mbunge badala ya  kushukuru  ameishia  kunilaumu  kuwa  kwanini nimeezeka nyumba na pesa nimepata wapi "

Hata   hivyo  Lyata  alisema  kwa  ajili ya kuonyesha ana  nguvu ya  kisiasa  kuliko  mbunge Mchungaji Msigwa ataendelea kufanya  siasa  na  kuwa suala la ubunge 2020 asubiri  muda  ufike  ila nyuma  yake  kuna  kundi  kubwa ya madiwani  na  viongozi wa chadema  watakaomfuata bila  kutaja majina  na  idadi yao  alisema  anaungwa mkono  na  madiwani  hao kwa uamuzi  wake .

Kuhusu  tuhuma  za  kununuliwa na  CCM kwa  zaidi ya  milioni 200 Lyata  alisema hajanunuliwa na kama amenunuliwa basi ni  mmoja  mwa  viongozi  wenye  sifa  kuzidi  ya  hao  wanaoeneza uvumi huu maana anayenunuliwa ni  yule anayekubalika na  aliyejiweka  jikoni kama  mmoja kati ya madiwani wa Chadema  ambae amekuwa  akieneza  uvumi ila huku  akitafuta  kununuliwa na  wana CCM

Kwa  upande  wake  Edga  Mgimwa  aliyekuwa  diwani wa  Kihesa  alisema  kuwa amevutiwa na kujiuzulu kwa Lyata  na  kuwa katika mkakati  wake  wa   kufanya kazi kama  kada wa CCM  jimbo la  Iringa ni madiwani  wengi  watajiuzulu .

Mbali ya Lyata na  Mgimwa  madiwani  wengine  waliojiuzulu kwa mwaka  jana na  sasa ni aliyekuwa diwani wa kata ya  Kitwiru  kupitia  Chadema  Baraka  Kimata  ambae  ni diwani  tena wa kata  hiyo  kupitia  CCM , pia  wapo madiwani  wa  viti maalum  wawili Husuna  Ngasi , Leah  Mleleu na  Lugano Mwanyingi

Mapema  mwaka jana akizungumza na  wanahabari mjini hapa  juu ya kujiuzulu kwa madiwani  wanne mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji Msigwa  ambae ni  mbunge  wa  jimbo  hilo  alisema  kuwa kuna  mkakati wa CCM kuendelea  kununua madiwani na  kukanusha malalamiko ya madiwani hao  kuwa yeye  ni  chanzo cha  wao kujiuzulu kwao .
Huku naibu  meya  wa Manispaa ya  Iringa  Dady  Igogo  alisema  kuwa chama  kimewanunulia  vifaa maalum   kwa  ajili ya madiwani wa Chadema wanaonunuliwa  kurekodi mazungumzo  ya  kununuliwa  kwao .

Msimamizi  wa  uchaguzi jimbo la Iringa  mjini  Omary  Mkangama ambae  ni kaimu  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa amethibitisha  kupokea  barua  za madiwani watatu ndani ya  wiki  hii  kutoka  Chadema  ambao  wamejiuzulu nafasi zao Tandesy  Sanga wa kata ya  Ruaha , Joseph  Lyata kata ya Kwakilosa na Anjelus Mbogo  wa kata ya Mwangata  .

"  Kwa  mujibu wa  sheria  nitamuandikia barua mstahiki  meya  ili  yeye  aweze   kumwandikia waziri mwenye   dhamana  ambae ataijulisha   tume  wa Taifa ya  uchaguzi  ili  taratibu  nyingine  zifanyike "

Alisema  jimbo la  Iringa  linazo kata 18   kati  ya  madiwani hao CCM  ina madiwani  watano  pamoja na yule wa  Kihesa  aliyepita  bila kupingwa  itakuwa na madiwani  sita   huku  Chadema   itabaki na madiwani  9.

Mwenyekiti  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)  Iringa mjini Frank Nyalusi asema atawatimua viongozi wote wanaotajwa na madiwani waliojiuzulu kuhusu hujuma zao kwa chama .
Amekiri  kuwa si shwali  ndani ya chama hicho kutokuwa  baada ya kasi ya kujiuzulu kwa madiwani wake hadi nane sasa huku mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa akitajwa kuwa chanzo cha kuua chama hicho.

Uchunguzi uliofanywa  unaonyesha kuwa viongozi wa chama hicho kwa sasa kila mmoja akimunyeshea kidole mwenzake huku mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Frank Nyalusi ambae alikuwa amesimamishwa na sasa ametangaza kurejea ameapa kutomfumbia macho kiongozi yeyote aliyehusika na kujiuzulu kwa madiwani hao kwa madai sababu za madiwani hao kujiuzulu zipo wazi hivyo mhusika ajiandae kuwajibika .

Nyalusi amesema kuwa kuna madiwani ndani ya Chadema wapo kwa ajili ya kuchafua wengine katika mitandao na kutuhumu kila mmoja kuwa amenunuliwa jambo ambalo si kwel;I ila na uwezo mdogo wa kufikiri mambo .

Alisema kuendelea kuwavumilia viongozi wapika majungu ndani ya chama hicho si sahihi na kuwa amepata taarifa ya mkutano wa kesho kuwa sehemu ya wapiga majungu kuendeleza maneo yao ya kuwatuhumu madiwani waliojiuzulu na kuwa kufanya hivyo si sawa .
" Hawa wanasiasa uchwara ni kuwapuuza mimi ndio mwenyekiti wa chadema Iringa mjini hivyo wengi wananiogopa narudi kurudi kusafisha mmoja baada ya mwingine... mimi niseme tu ukipanda mabaya unavuna mabaya na mshahara wa dhambi ni mauti kinachoendelea Chadema Iringa mjini ni mavuno ya ubaya  ambayo mbegu yake ilipandwa Matendo ambayo walinitendea mimi sasa wanasiasa uchwara wanaibuka nisema huenda 2020 nitachukua fomu "

Nyalusi asema CCM si kweli inanunua madiwani wa Chadema ila CCM imewazidi ujanja Chadema isipokuwa kila  chama  kina mkakati  wake wa kupata  idadi kubwa ya  wanachama .

Akiwa katika mkutano  wake Mlandege  mbunge  Msigwa alisema wote  wanaotaka  kuondoka  Chadema  waondoke  kwani yeye  alikuwa ni  mbunge pekee  katikajimbo hilo kwa  upinzani hivyo wanaoendelea  kujiuzulu  wajiuzulu  .

Kujiondoa kwa madiwani hao kunaifanya Chadema iliyonyakua viti 14 kati ya 18 vya udiwani katika jimbo hilo mwaka 2015 na kufanikiwa kubeba halmashauri ya manispaa ya Iringa, kubakiwa na madiwani nane ambao pia hakuna mwenye uhakika kama wote wataendelea kuzitumikia nafasi hizo hadi mwaka 2020 utakapofanyika uchaguzi mkuu mwingine.

Wakati Chadema ikibakiwa na madiwani nane wa kuchaguliwa, Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wake kimeongeza idadi ya madiwani kutoka wanne hadi sita hiyo ikiwa ni baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo katika kata ya Kitwiru na mgombea wake kupita bila kupingwa katika kata ya Kihesa.

Aidha CCM inatarajia kushinda katika kata zingine nne zilizowazi hasa kwa kuwa Chadema kwa kupitia Mwenyekiti wake Freeman Mbowe ilikwishatangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wowote kwa madai kwamba chaguzi hizo haziko huru na haki; jambo litakaloifanya iwe katika nafasi nzuri ya kuongeza madiwani wake hadi 10.

Tarifa za kujiuzulu kwa madiwani wa Chadema kunazidi kupokelewa kwa nderemo na vifijo na wanachama na viongozi wa CCM.

Mwenyekiti wa CCM wa Manispaa ya Iringa Said Rubeya alisema; “Hatukuamini macho yetu tulipopoteza jimbo na halmashauri katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na sasa hatuamini macho yetu jinsi yanavyoshuhudia madiwani wa Chadema wakijiengua katika chama hicho.”

Rubeya alisema kwa maamuzi hayo ya madiwani wa Chadema, CCM inajiona ipo katika mazingira mazuri ya kuirudisha halmashauri ya manispaa ya Iringa katika mikono yake.

“Endapo Chadema itapoteza madiwani wengine wawili, hakuna shaka meya wa sasa atakuwa amepoteza mamlaka ya kuendelea kukikalia kiti hicho na hivyo baraza la madiwani wa manispaa ya Iringa litalazimika kuchagua meya mwingine na endapo itakuwa hivyo hakuna shaka CCM watakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa kiti hicho,” alisema.

Akizungumzia hamahama ya madiwani wao na hatma yake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe alisema jambo hili linawaumiza wapenda mageuzi wengi kwani walipowachagua madiwani kutoka upinzani hawakujua kama hatma yake itakuwa kutoswa katikati ya njia.

“Walipoanza kuondoka na kujiunga na CCM, tumekuwa tukifanya vikao, bahati mbaya madiwani wanaohama, wamekuwa wakiapa mbele ya vikao kwamba hawana sababu na hawawezi kufanya hivyo. Lakini yanayotokea ndio hayo,” alisema.

Kama Meya wa manispaa hiyo alisema anaiona dalili ya kupoteza kiti hicho kwa CCM lakini akajipa moyo akisisitiza; “sikuzaliwa kuwa meya na kwamba hayo ni majukumu ya kupokezana ambayo matokeo yake uamriwa kwa kura.”

“Ombi kwa wanamageuzi wenzangu, tusikate tamaa, kuna kimbunga cha ajabu kinapita katika chama chetu, tukumbuke hakuna jambo lisilo na mwisho, nina hakika mambo yatakaa sawa,” alisema huku akisisitiza kwamba hafikirii kuhama chama hicho kama walivyofanya madiwani wenzake na akawaomba pia wenzake waliobaki wasiwakimbie wapiga kura wao kwa kuhama chama hicho.

Akizungumza na wanahabari, diwani aliyejiuzulu alisema; “Nimeamua kujiuzulu kwa hiari yangu mwenyewe baada ya kuona napoteza muda mwingi katika nafasi hii na kwa kuzingatia ahadi nyingi nilizotoa wakati wa uchaguzi mkuu uliopita sasa zinatekelezwa na serikali ya Dk John Magufuli kwa kasi kubwa.”

Kwa muktadha huo, Kafuka alisema haoni tena sababu ya kuendelea na wadhifa huo na kujishughulisha na mambo ya kisiasa kwasasa na badala yake anataka kuitumia familia yake na kuendeleza shughuli zake za ukandarasi zilizoanza kuyumba baada ya kuwa diwani.

“Nichukue nafasi hii kuwashukuru wananchi wa kata yangu na manispaa ya Iringa kwa ushirikiano walionipa katika kipindi nilichokuwa diwani wao na kufanikiwa kutekeleza majukumu mbalimbali ya kuwaletea maendeleo,” alisema

Msimamizi  wa  uchaguzi jimbo la Iringa  mjini  Omary  Mkangama ambae  ni kaimu  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa amethibitisha  kupokea  barua  za madiwani watatu ndani ya  wiki   iliyopita kabla  ya jana  kuongezeka  wa  nne wa kata ya Mkwawa kutoka  Chadema  ambao  wamejiuzulu nafasi zao Tandesy  Sanga wa kata ya  Ruaha , Joseph  Lyata kata ya Kwakilosa , Anjelus Mbogo  wa kata ya Mwangata na Mkwawa Oscar Kafuka  .

"  Kwa  mujibu wa  sheria  nitamuandikia barua mstahiki  meya  ili  yeye  aweze   kumwandikia waziri mwenye   dhamana  ambae ataijulisha   tume  wa Taifa ya  uchaguzi  ili  taratibu  nyingine  zifanyike "

Alisema  jimbo la  Iringa  linazo kata 18   kati  ya  madiwani hao CCM  ina madiwani  watano  pamoja na yule wa  Kihesa  aliyepita  bila kupingwa  itakuwa na madiwani  sita   huku  Chadema   itabaki na madiwani  8 .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE