January 6, 2018

KUJIUZULU KWA MADIWANI IRINGA MJINI, FRANK NYALUSI KIKIVURUGA MBUNGE MSIGWA MGUU NDANI MGUU NJE UBUNGE 2020 ...HALI  ya  mambo  ndani ya  chama  cha  Demokrasia  na maendeleo (Chadema)  Jimbo la  Iringa  mjini si  shwali  baada ya  kasi ya  kujiuzulu  kwa  madiwani  wake hadi  kufikia  madiwani   saba   sasa huku  mbunge  wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji  Peter  Msigwa  akitajwa  kuwa  chanzo  cha  kuua  chama   hicho.

Uchunguzi  uliofanywa na matukiodaima  unaonyesha  kuwa  viongozi  wa  chama  hicho  kwa  sasa  kila  mmoja  akimunyeshea  kidole  mwenzake   huku mwenyekiti  wa Chadema   wilaya ya  Iringa mjini  Frank Nyalusi  ambae  alikuwa  amesimamishwa na  sasa  ametangaza  kurejea  ameapa  kutomfumbia macho  kiongozi   yeyote  aliyehusika  na kujiuzulu kwa madiwani  hao kwa madai  sababu  za  madiwani  hao  kujiuzulu  zipo  wazi  hivyo  mhusika ajiandae kuwajibika .

Akizungumza  katika mahojiano maalum  leo  na matukiodaima  Nyalusi  amesema  kuwa kuna  madiwani  ndani ya  Chadema  wapo  kwa  ajili ya  kuchafua wengine  katika  mitandao  na  kutuhumu  kila  mmoja  kuwa  amenunuliwa  jambo  ambalo  si  kwel;I  ila  na  uwezo  mdogo  wa  kufikiri  mambo .

Alisema  kuendelea  kuwavumilia viongozi  wapika majungu ndani ya  chama  hicho  si  sahihi na kuwa  amepata taarifa  ya mkutano  wa  kesho  kuwa  sehemu ya wapiga majungu  kuendeleza maneo yao ya  kuwatuhumu  madiwani  waliojiuzulu  na kuwa  kufanya  hivyo  si   sawa .

"  Hawa  wanasiasa  uchwara  ni  kuwapuuza  mimi  ndio mwenyekiti  wa chadema  Iringa mjini hivyo  wengi  wananiogopa narudi  kurudi  kusafisha  mmoja baada ya  mwingine... mimi  niseme  tu ukipanda mabaya  unavuna mabaya na mshahara  wa   dhambi ni mauti  kinachoendelea  Chadema Iringa mjini  ni  mavuno  ya  ubaya  ambayo mbegu  yake  ilipandwa  Matendo  ambayo walinitendea  mimi sasa  wanasiasa  uchwara  wanaibuka nisema  huenda 2020  nitachukua  fomu  "


Nyalusi asema  CCM si  kweli inanunua madiwani  wa Chadema  ila CCM  imewazidi  ujanja  Chadema .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE