January 9, 2018

Korea Kaskazini na Korea Kusini zaanza mazungumzo ya kihistoria baada miaka 2


Korea Kaskazini na Korea Kusini wameanza mazungumzo ya Olimpiki
Haki miliki ya picha

Waziri wa muungano wa Korea Kusini , Cho Myoung-Gyon amesema mazungumzo hayo yanajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na kutumia fursa hiyo kuimarisha uhusiano.
"Tutahudhuria mkutano huu ili kuzungumzia suala la korea kaskazini kushiriki katika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yatayofanyika korea kusini na kuimarisha uhusiano wan chi hizi mbili.Ninaelewa kuwa matarajio ya wengi juu ya mkutano huu ,kwanza ni kuhusu mawasiliano baina ya nchi hizi mbili ambayo yalisitishwa kwa muda.Tuna lengo la kufanya mashindano haya ya Olimpiki kuwa ya hatua ya kwanza ya kuboresha Amani baina ya nchi hizi mbili hivyo hii ni hatua nzuri na hatuna haraka."Cho Myoung-Gyon aeleza.
Uhusiano kati ya nchi hizo mbili uliporomoka baada ya Korea Kusini kukatisha mradi wa pamoja wa kiuchumi huko eneo la kiuchumi la Kaesong Korea Kaskazini, na kufuatiwa na majaribio ya nyuklia yaliofanywa na Korea Kaskazini.
simuHaki miliki ya picha
Image caption
Mazungumzo ya mwisho baina ya nchi hizo mbili yalifanyika Disemba mwaka 2015 huko Korea ya Kusini.
Siku ya Jumatatu waziri wa muungano wa Korea Kusini alisema kuwa mazungumzo hayo yatajikita zaidi katika masuala ya olimpiki lakini mambo mengine pia yatajadiliwa.
''wakati tunazungumzia mausala ya uhusiano wa korea, serikali itazungumzia pia suala la matokeo ya vita na njia za kupunguza mvutano wa kijeshi'' alisema waziri Cho Myoung-gyon ambaye ataongoza mazungumzo hayo yatakayohudhuriwa na wawakilishi watano.
Nayo Korea Kaskazini watatuma wawakilishi watano wakiongozwa na Ri Son-gwon ambaye ni mwenyekiti wa Idara ya serikali ya Korea ya Kaskazini mwenye dhamana ya masuala na Kusini.
Mkutano huo utafanyika katika kijiji cha PanmunjomHaki miliki ya picha

Kijiji hicho hujulikana kama kijiji cha pande mbli, ambapo kila upande una miliki sehemu yake na katikati kuna jengo la umoja wa mataifa. Baada ya vita ya korea kuisha mwaka 1953 kijiji cha Panmunjom kiliamuriwa kuwa sehemu ya pande zote mbili, na maofisa wa pande wanaweza kukutana hapo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE