January 10, 2018

KIFO CHA OMARY KAPERA RAIS KARIA ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

DMMJc-BXUAYMJCD.jpg large

Kufuatia kifo cha beki wa zamani wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Omary Kapera,Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya kifo cha beki huyo wa zamani.
Rais Karia akitoa salamu za rambirambi amesema ni masikitiko makubwa kumpoteza mmoja wa wachezaji wa zamani aliyeitumikia pia timu ya taifa.
“Nimeshtushwa na taarifa hizo za kifo cha Kapera hasa ikichukuliwa bado tupo kwenye majonzi ya kumpoteza mchezaji mwingine wa zamani Athuman Juma Chama,kwa niaba ya Shirikisho natoa pole kwa wote walioguswa na msiba huo kuanzia kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki.”Alisema Rais Karia.
Wakati wa uhai wake akicheza mpira amecheza katika klabu za Pan Africans na Yanga huku akipata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars”
Kufuatia msiba huo TFF itatoa rambirambi kwa familia ya Kapera.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE