January 5, 2018

KASI YA MADIWANI JIMBONI KWA MCHUNGAJI MSIGWA KUJIUZULU INATISHA , YUPO KATIBU WA CHADEMA MKOA

Diwani  wa kata ya  Mwangata Anjelus Mbogo kushoto   akizungumza na  wanahabari  leo  baada ya  kujiuzulu kwake wengine ni katibu kata  ya  Mwangata Tumaini Gwivaha  na aliyekuwa katibu wa mkoa wa Iringa Chadema Oscar Ndale  ambao  wote  wamejiuzulu  leo
Katibu wa  Chadema  mkoa wa Iringa Oscar Ndale  katikati  akiwa na diwani wa Mwangata  Anjelus Mbogo na katibu kata  ya  Mwangata  Tumaini Gwivaha  baada ya  kujiuzulu  leo

Na MatukiodaimaBlog
IDADI ya  madiwani  wa  chama  cha  Demokrasia na  maendeleo  (chadema)  jimbo la  Iringa  mjini  kujiuzulu  imezidi  kuongezeka   na  kufikia madiwani  saba   sasa  baada ya watatu kujiuzulu ndani ya  wiki  hii pamoja  na katibu  wa chadema mkoa  wa Iringa  Oscar Ndale  .

wakati diwani wa Kwakilosa na Ruaha  walijiuzulu kwa pamoja    juzi diwani  wa Mwangata  Anjelus Mbogo alijiuzulu leo   pamoja na  katibu  wa mkoa  wa  chama  hicho  na katibu  kata  wa  Chadema Mwangata  Tumaini Gwivaha .


wakitangaza  azma  ya  kujiuzulu  kwao nafasi hiyo   mbele ya waandishi  wa  habari  Mbogo  na  Ndale  walisema   kuwa  kujiuzulu  kwao kumetokana na mahusiano mabaya  ya  kufifisha maendeleo  kwenye kata  yake pamoja na mabavu  ya  viongozi w juu wa Chadema .

kati  yake na  viongozi wa  juu wa Chadema  hicho akiwemo  mwenyekiti wa kanda ya  Nyasa Mchungaji  Peter  Msigwa  ambae  ni  mbunge wa   jimbo  la  Iringa mjini pamoja  na  uongozi wa juu wa Chadema  ukiongozwa na mwenyekiti  wake  Taifa Freeman  Mbowe.


"  Vyama  vya  siasa  vipo  vingi  kuna  CUF , ACT  Wazalendo  na  CCM  hivyo  nitachagua  ni  chama gani  kitanifaa  kufanya  siasa  zangu ila  hata  CCM nipo  tayari  hakuna  ubaya "

Alisema  kuwa  mbunge Msigwa  amekuwa  akimfanyia  diwani  mwenzao Joseph Lyata figisu  figisu toka  akiwa naibu meya  wa Manispaa ya  Iringa na  hofu ya mbunge  Msigwa  ni baada ya  kuhisi kuwa anautafuta  ubunge wa  jimbo  hilo mwaka  2020 .

Diwani  Mbogo alisema  kwa  sasa atabaki  mwanasiasa   huru  na  iwapo  mbunge  Msigwa na mstahiki meya  Alex Kimbe wataondoka  hata  leo  chadema basi atarejea  Chadema  ila  kama   wataendelea  kubaki hatarudi  kamwe .

Kwa  upande  wake aliyekuwa  katibu  wa Chadema  mkoa ,Ndale  alisema  kuwa kuyumba  kwa chadema  Iringa mjini  kumesababishwa na mbunge   kutokuwa na ushirikiano mzuri  na  wenzake na mara  kadhaa  wamekuwa  wakimuonya ila  bado  anaendelea  na kuwa  Mbowe pia  amesababisha  kujiuzulu kwake  nafasi hiyo  na  kwa  sasa  atajiunga na  CCM .

Ndale  alisema aliomba kujiunga na  CCM na amekubaliwa na  hivyo ataendelea na  Siasa  kupitia CCM huku akisema uhai  wa Chadema  Iringa  mjini  umefika  mwisho .

Kwa  upande  wake Joseph Lyata  aliyekuwa  diwani kata ya  Kwakilosa  alisema siasa ndani ya  Chadema kwake  imemshinda hivyo ameamua  kuondoka  ndani ya  chama  hicho na  kuwa  mwanasiasa  huru .

Msimamizi  wa  uchaguzi jimbo la Iringa  mjini  Omary  Mkangama ambae  ni kaimu  mkurugenzi wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa amethibitisha  kupokea  barua  za madiwani watatu ndani ya  wiki  hii  kutoka  Chadema  ambao  wamejiuzulu nafasi zao Tandesy  Sanga wa kata ya  Ruaha , Joseph  Lyata kata ya Kwakilosa na Anjelus Mbogo  wa kata ya Mwangata  ."  Kwa  mujibu wa  sheria  nitamuandikia barua mstahiki  meya  ili  yeye  aweze   kumwandikia waziri mwenye   dhamana  ambae ataijulisha   tume  wa Taifa ya  uchaguzi  ili  taratibu  nyingine  zifanyike "

Alisema  jimbo la  Iringa  linazo kata 18   kati  ya  madiwani hao CCM  ina madiwani  watano  pamoja na yule wa  Kihesa  aliyepita  bila kupingwa  itakuwa na madiwani  sita   huku  Chadema   itabaki na madiwani  9.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE