January 7, 2018

JORDAN YATAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUITAMBUA PALESTINA KUWA TAIFA

Image result for JORDAN YATAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUITAMBUA PALESTINA KUWA TAIFAJordan imesema jumuiya ya nchi za Kiarabu itatafuta ridhaa ya Jumuiya ya Kimataifa kuitambua Palestina kama taifa na Jerusalem Mashariki kuwa mji mkuu wake baada ya Marekani kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel mapema mwezi uliopita na kuibua ghadhabu kwa Palestina, katika mataifa ya Kiislamu na katika jumuiya ya Kimataifa kwa jumla.
Waziri wa mambo ya nje wa Jordan Ayman Sfadi aliyatangaza hayo baada ya kukutana na kiongozi wa jumuiya ya nchi za Kiarabu Ahmed Abul Gheit mjini Amman kujadili suala hilo la Jerusalem.
Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje wa Misri, Saudi Arabia, Morocco, Umoja wa Falme za Kiarabu na Mamlaka ya ndani ya Palestina.
Abul Gheit amesema mkutano mkubwa wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Kiarabu kujadili hatma ya mji wa Jerusalem utafanyika mwishoni mwa mwezi huu. Jerusalem ni mojawapo ya masuala tete katika mzozo kati ya Israel na Palestina.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE