January 2, 2018

Israel yawataka wahamiaji kutoka Afrika kuondoka nchini humo

        Wengi wanatoka Eritrea na Israel                           

Serikali ya Israel imetoa ilani ya siku tisini kwa maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika kuondoka nchini humo au kuhukumiwa kifungo.
Utaratibu huo utaathiri wanaotafuta hifadhi ambao watalazimishwa kurudi nchi zao au kupelekwa Uganda au Rwanda.
Mwandishi wetu wa BBC Emmanuel Igunza anasema wengi wa wale watakaoathirika ni wale walioshindwa kupata hifadhi hasa raia wa Eritrea na Sudan ambao ndio idadi kubwa ya wahamiaji nchini Israel.
Taarifa kutoka Mamlaka ya Wahamiaji ya Israeli inasema wahamiaji wote wanapaswa kuondoka nchini kufikia mwishoni mwa mwezi Machi.
Kila mmoja wao atapata shilingi ya $ 3,500 au kurudi nchi zao za nyumbani au kuhamishwa hadi Rwanda au Uganda.
Hata hivyo, utaratibu huu hautawahusisha watoto, wazee na waathirika wa utumwa na usafirishaji wa binadamu.
Serikali ya Israel inasema mradi huo ni wa hiari na utakuwa utu.
Wahamiaji kutoka Afrika                           
Lakini shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa na makundi mengine ya haki za binadamu yanasema mipango hiyo ya utata inakiuka sheria za kimataifa na zile za Israel.

Israeli kwa muda mrefu imejaribu kukabiliana na maelfu ya Waafrika wasiokuwa Wayahudi wanaoiingia nchini humo, wakitafuta hifadhi au kazi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE