January 29, 2018

ILIPOFIKIA KESI YA MEYA WA MANISPAA YA IRINGA ALEX KIMBE

Kesi Inayomkabili Meya Wa Manispaa Ya Iringa Alex Kimbe Ya Kutishia  Kuua Kwa Bastola Wakati Wa Uchaguzi Mdogo Wa Novemba 26, 2017  Inatazamiwa Kuanza Kusikilizwa Baadae Februali Tano Mwaka Huu Baada Ya Upelelezi Kukamilika.

Akizungumza Mbele Ya Hakimu Wa Wilaya Ya Iringa John Mpitanjia Mwendesha Mashtaka Wa Serikali Alex Mwita Amesema Upelelezi Wa Shauri Hilo Lenye Usajili Wa Namba 189 Ya Mwaka 2017  Umekamilika Hivyo Tarehe Hiyo Itaanza Kusikizwa Mwezi Ujao.

Kimbe Katika Kesi Hiyo Anatuhumiwa Kumtishia Kumuua Kwa Bastola Katibu Wa Umoja Wa Vijana Wa Chama Cha Mapinduzi (Uv Ccm) Manispaa Ya Iringa, Alphonce Muyinga Kinyume Na Kifungu Namba 89 (2) (A) Cha Kanuni Za Adhabu Katika Kata Ya Kitwiru Mjini Iringa Wakati Shughuli Ya Uchaguzi Mdogo Wa Udiwani Wa Kata Hiyo Ikiendelea.

Tofauti Na Siku Za Kabla Meya Ambaye Hakutaka Kujumuishwa Kwa Wakili Katika Kesi Yake Leo Aliwasili Mahakamani Hapo Akiwa Na Ujumbe Wa Viongozi Wa Chama Anachotokea Cha Chadema Pamoja Na Wanachama.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE