January 12, 2018

GLOBAL IMETAJA LIST YA MASTAR WANAODEKEZANA ZAIDI HADHARANI

KWENYE uhusi-ano, kila mmoja ana staili yake. Kuna ambao huwa wanapenda kuanika mambo yao hadharani, kuna wengine wanafanya uhusiano wao kuwa siri.
Wapo mastaa ambao wamekuwa wakioneshana mahaba niue hadharani tena zaidi wapo wanaokwenda mbali zaidi kwa kuonesha jinsi gani wanavyodeka wanapokuwa na wenzi wao.
Kwa kawaida huwezi kumpangia mtu jinsi ya kuishi na ndiyo maana mastaa mbalimbali wamekuwa wakiweka picha zao katika mitandao ya kijamii, japo mara kadhaa wamekuwa wakikutana na changamoto ya matusi.
Katika makala haya tunakuletea mastaa vinara wa kudekezana wawapo na wenzi wao:
ROMA
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa ‘Roma’ na mke wake, Nancy Mshana wamekuwa wakionyeshana mahaba niue hadharani bila kujali macho ya watu ambapo wamekuwa wakiachia picha zao wakiwa kimahaba zaidi.
Mke wa Roma amekuwa akionesha ni jinsi gani anavyodekezwa na mumewe huyo kutokana na wanavyokuwa wanapokuwa pamoja na kujidhihirisha wanavyopendana hali ambayo inamfanya pia apongezwe sana mitandaoni japo baadhi humkosoa.
AUNT EZEKIEL
Staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel huyu anaonekana ni bingwa wa kudeka awapo na mpenzi wake kwani siku za hivi karibuni picha zilisambaa akiwa amebebwa mgongoni na mpenzi wake ambaye ni baba mtoto wake, Moses Iyobo.
Picha hiyo ilionekana kuwa kivutio katika mitandao ya kijamii na siyo hiyo tu zipo picha nyingi zinazomuonyesha mwanamama huyo akideka kwa mwenzi wake huyo.
SHILOLE
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ambaye ni mke wa ndoa wa Ashrafu Uchebe amekuwa akimdekea vilivyo mpenzi wake huyo huku wakati mwingine naye akidekewa na mwanaume huyo.
Wawili hawa wamekuwa kama kumbikumbi kwani mara nyingi wanakuwa pamoja sehemu mbalimbali iwe kwenye mgahawa anaomiliki mwanamuziki huyo au msikitini wanakwenda pamoja.
Shilole na mumewe wamekuwa wakiachia picha zao kwenye mitandao ya kijamii wakiwa wanaoneshana mahaba huku mwanaume akimsifia kila wakati mkewe huyo ambapo anakutana na matusi kibao kutoka kwa mashabiki.
MR BLUE
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Herry Sameer ‘Mr Blue’ naye anaingia kwenye listi kwa kuwa muda mwingi anaonesha kudeka huku mkewe, Wayda naye akimdekea vilivyo jambo ambalo linawaongezea mvuto katika penzi pamoja na familia yao.
VANESSA
Staa wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee akiwa na mpenzi wake utamsahau kwani anakuwa anadeka vilivyo na kuwa kimahaba zaidi mithili ya mtoto mdogo.
Vanessa na mpenzi wake Jux wanapokuwa pamoja wamekuwa wakioneshana mahaba ya aina yake na kuonesha ni jinsi gani Jux anavyom-dekeza mwanadada huyo ambaye waliachana na kurudi-ana.
Gladness Mallya | RISASI

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE