Familia ya marehemu kijana David Wokabi ambaye alikuwa akifanya kazi benki nchini Kenya, imerudisha mwili wa marehemu huyo mahali ambapo alipigwa na watu waliosababisha kifo chake, ili kudai haki na fidia. 
Marehemu David Wokabi
Msemaji wa familia amesema David alikuwa na majukumu yake, kwa hivyo kifo chake kimewapa wakati mgumu wa kuhudumia familia yake.
“Tumeleta huu mwili hapa kwa sababu damu yake ilimwagwa hapa, kama wanataka kumla wamle lakini sisi familia tuna watoto wawili na mke wa marehemu, Alikuwa na majukumu yake, kwa hiyo tunaiomba serikali itende haki kwa sbabau kuna watoto wa miaka miwili na mitatu, ambao hatujui nani atawahudumia”, amesema Msemaji huyo ambaye jina lake halikutajwa kwa mara moja.
Davidi alipigwa na walinzi watano wa benki hiyo kwa kosa la kukojoa kwenye parking ya magari, alifariki siku saba zilizopita, akiwa hospitali kwenye chumba cha wagonjwa mahututi alipokuwa akiuguza majeraha aliyoyapata kwa kipigo.
Camera za ulinzi za CCTV zimeonyesha walinzi hao wakimtoa David Wakobi kwenye gari lake alipokuwa akianza kutoka sehemu ya parking na kumvuta nje, na kisha kuanza kumshushia kipigo kilichomuacha na hali mbaya kiafya.
Tayari jeshi la Polisi limewakamata watu wawili kufuatia tukio hilo, huku wengine watatu wakikimbilia kusikojulikana huku wakiendelea na msako wa kuwakamata.