January 22, 2018

DR MOLLEL; NILIFANYA JAMBO LA KITOTO AWALI

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Siha kwa tiketi ya CHADEMA, Godwin Ole Mollel ambaye alihama chama hicho na kujiunga na CCM amefunguka na kusema alipotoka Bungeni wakati Rais Magufuli anaingia ulikuwa ni uamuzi wa kitoto.
Mollel amesema hayo jana wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi wa marudio ambao unatarajiwa kufanyika Februari 17, 2018 ambapo Mollel sasa anagombea ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Nilipofika Bungeni nikaambiwa ukimuona Magufuli anaingia Bungeni wewe toka nje, nikabisha kidogo nikaambiwa wewe ambaye ni mbishi kwanza tangulia mbele, kwa sababu mimi nina nidhamu na naheshimu viongozi nikatangulia kikamanda mbele nikatoka nje, nikiumia nikisema nimefanya jambo la kitoto lakini ikafika mahali nikaambiwa hauruhusiwi kuongea na Mbunge wa CCM, wala kumsalimia" alisema Mollel
Mbali na hilo Mollel anasema baadaye aliambiwa ashone suti ili siku bajeti ikiwa inajadiliwa watoke nje lakini yeye anadai aligoma na kuanzia hapo alianza kuchukiwa ndani ya chama chake hicho alichokihama.
Pia Mollel amedai kuwa anatambua Lowassa atakuja kupiga kampeni za CHADEMA Siha na kusema anatambua kiongozi huyo amepangwa na hawezi kukataa kwa kuwa anaogopa kufukuzwa kwenye chama kwa kuwa tayari yeye ni mzee lakini amesema alishawaeleza ukweli kutoka Ikulu kwamba CCM ndiyo mpango.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE