January 30, 2018

DC KILOLO AZINDUA KILIMO CHA ZAO LA KOROSHO ,AONYA WATAKAOZEMBEA

Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  mkoani Iringa Asia Juma Abdalah akipanda  mche  wa korosho baada ya kuzindua kilimo  cha zao  hilo katika  kijiji cha Magana tarafa ya  Mahenge jana
Miche  ya  korosho  iliyooteshwa ikiwa  tayari  kutolewa  bure kwa  wananchi
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Juma  Abdalah kushoto  akiwa na   viongozi  mbali mbali  wa Kilolo  wakitazama vitalu  vya  miche ya  Korosho itakayotolewa  bila malipo kwa  wananchi
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Juma Abdalah  akichimba  shimo la  kupanda  mche wa  korosho
Mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Asia Juma Abdalah  akiwahutubia  wananchi wa kijiji  cha Magana  wakati wa  uzinduzi wa kilimo  cha  zao la Korosho
Mkuu  wa  wilaya  Asia Abdalah  akisisitiza  jambo wakati wa  mkutano  huo
Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia  Juma Abdalah  akizindua  rasmi  kilimo cha  zao la  Korosho
SERIKALI  ya  wilaya ya  Kilolo  mkoani  Iringa imetoa  onyo  kwa  wakulima
wataoshindwa  kutunza miche ya korosho iliyotolewa bure  na serikali ya
Rais Dkt John Magufuli kwa lengo la  kuanzisha  kilimo  hicho.

Pamoja  na kuwaonya wakulima kutozembea  kutunza miche  hiyo pia
maofisa   kilimo
ama  watendaji  wa  serikali  ngazi ya  vijiji  na kata watakaobainika
kuwauzia  miche wakulima kuwajibishwa .

Onyo  hilo  limetolewa na mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Asia Abdalah   wakati
akizindua upandaji  wa zao la korosho  katika  kijiji  cha Magana  kwa
tarafa  ya  Mahenge wilayani  humu  jana .

Alisema  kuwa  kila  mwananchi atapewa  bure  miche  kuanzia  30  kwa  ajili
ya  kupanda  heka  moja  na ambao watakuwa na  ardhi  kubwa  zaidi
watajiandikisha  ili  kuongezewa  miche zaidi  kulingana na ukubwa  wa ardhi
yake .

“ Ardhi heka  moja  ukiitumia  vizuri   wewe ni  tajiri hapa  miongoni
mwetu  wapo ambao  wana ardhi  kuanzia  heka  moja  hadi  500 ambazo
hazitumiki   kwa  kilimo  hivyo  kupitia mradi   huu  wazao la  korosho
pandeni miche  ya  korosho  ambayo  itawezesha  kukuza  uchumi  wenu”

Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema  hapendi  kuona  ugonjwa  wa  umasikini
ukiendelea  miongoni  mwao  kwani jitihada  za  Rais  hadi  kufikia hatua ya
kuwapatia  miche   hiyo  ni  kutaka  wananchi  kuwa na kipato.

“  Mkipewa  miche  hakikisheni  mnaipanda  na  kuitunza  vema kwa  kuwasikiliza
maofisa  kilimo ili  kuulinda  usife  nilishawaeleza kama utashindwa
kutunza  mche ni  vizuri  ukaacha  usichukue  ili wenye  uhitaji  waweze
kuchukua  tena  naagiza  diwani na afisa  kilimo  pamoja na mtendaji  wa
kijiji  kuwepo  kwamkataba  kwa  kila mmoja ili atakayeshindwa kutekeleza
mkataba  tuwajibishane”

Aidha  mkuu  huyo wa  wilaya  aliwataka  wananchi kupanda  miche   hiyo
katika ardhi zao halali na  wale  wasio na ardhi  basi  kupewa  miche  ya
kupanda kuzunguka  nyumba  wanazoishi na  sio kupitia  kilimo hicho  cha
korosho  kuanza  kuibuka kwa  migogoro  ya ardhi katika  kijiji hicho .

Asia  aliwataka maofisa  kilimo wa  kata  hadi  wilaya  na  vijiji
kutoka  maofisini
na  kwenda mashambani  kuwasaidia  wananchi  kupata  elimu   ya  kilimo  cha
zao hilo la Korosho na  kuwa wilaya  ya  Kilolo kwa  sasa  inayo mazao
matatu  ya  biashara  ambayo  yanahamasishwa kulima  ambayo ni Chai ,
Parachichi  na zao la  Korosho .

Afisa  Kilimo  wa wilaya  ya  Kilolo  Shehemba Kuziwa  alisema hadi sasa
pamoja na miche hiyo ya kijiji  cha Magana  kuna jumla ya  miche 45,228
itakayotosha  hekta 646 hivyo  kila mwananchi  aliyetayari kulima atapewa
bure  miche   hiyo  .

Alisema  kuwa Halmashauri  ya  Kiloloimeweka  mkakati  wa kutekeleza  agizo
la  viwanda  kwa  kufufua  mazao  mbali mbali na  kuwa  kwa  kushirikiana
na bodi ya  korosho  wamekuwa  wakiendesha  mradi wa korosho  Kilolo .

Alisema  wananchi  wameweza  kushiriki  kuotesha  miche   hiyo ambayo  mbegu
ilitolewa na bodi ya  korosho  na  kuna  vikundi  vitano  na  taasisi  mbali
ambazo  zinahusika  kuotesha miche .

Afisa  ugani wa kijiji  cha Magana  Justine  Kitalima  alisema  kuwa
walipokea  mbegu  kilo  52 ambayo  sawa na  7512 ila  baada ya  kuzalisha
wamepata  miche  61200  ambayo  imepona katika  kijiji  hicho .

Aidha  alisema  wananchi  wamepokea kilimo  hicho    kwa  mwitikio mkubwa
zaidi  hasa  ukizingatia  kuwa  awali  wananchi  wachache  walikuwa  wakilima
zao  hilo kabla ya  kuacha  kutokana na changamoto ya  soko  ila  sasa  baada
ya soko  kuwa la uhakika  wengi  wanahamasika  kulima  zao   hilo.
TAZAMA  VIDEO ZOTE HAPA  CHINI 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE