January 25, 2018

DC KILOLO AIPONGEZA ASAS YA MMADEA ATAKA IZIDI KUTOA ELIMU YA ARDHI

Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah kushoto akifungua kikao cha MMADEA leo


Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah wa pili kushoto akiwa na viongozi wa MMADEA pamoja na mwakilishi  mkurugenzi Kilolo  Elias Naminga kulia 
Washiriki wa kikao hicho .
,.....................................

Na Matukiodaimablog 

MKUU wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ameitaka taasisi isiyo ya kiserikali ya Mazombe Mahenge Development ( MMADEA) kusaidia kutoa elimu ya ardhi wilayani humo ili kukomesha kero ya migogoro ya ardhi .


Mkuu huyo wa wilaya alitoa rai hiyo Leo  wakati akifungua kikao cha mrejesho wa utekelezaji wa mradi wa asasi ya MMADEA kwenye wilaya hiyo.

Alisema kuwa suala la migogoro ya ardhi kwenye wilaya yake ni kero kubwa kutokana na kasi kubwa ya wananchi kupenda kuuza ardhi yao kwa wageni.

Kuwa kutokana na uuzaji huo holela wa ardhi katika maeneo Mengi ya wilaya kumekuwa na migogoro zaidi ya ardhi huku wajane na watoto wakiongoza kwa kupokonywa ardhi yao.

"Pamoja na kazi nzuri ambayo MMADEA mnaifanya nawaombeni sana endeleeni kutoa elimu katika wilaya ya Kilolo hasa ya uuzaji holela wa ardhi maana wananchi wamekuwa wakiuza ardhi ovyo na kuzusha migogoro isiyo Kwisha ya ardhi"

Pia mkuu huyo wa wilaya aliitaka jamii ya wanakilolo kuepuka kuuza ardhi yao kwa wageni kwani kwa kuedelea kuuza ovyo ardhi kutapelekea baadae watoto wao kuja kukosa ardhi ya kulima.

Kuhusu elimu iliyotolewa na upangaji wa bajeti shirikishi kwa kuanzia ngazi za chini elimu iliyotolewa na asasi hiyo ya MMADEA alisema elimu hiyo itawezesha kukuwa kwa uwajibikaji kwa wananchi na kuongeza ufanisi shirikishi utakao mfanya Rais John Magufuli kuendeleza jitihada za kuwatumikia wananchi.

Alisema azma ya Rais ni kuona wananchi wote wananufaika na matunda ya nchi hii na kuwa iwapo kila mmoja atafanya kazi kwa juhudi kubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa MMADEA Raphael Mtitu alisema wamefanikiwa kutoa elimu kwa jamii ya Kilolo na sehemu kubwa kero za ardhi zimeanza kupungua baada ya kuwa na elimu .

"Tulichojifunza wanawake wakishirikishwa kikamilifu kwenye shughuli za maendeleo wana michango mingi yenye tija kwa maendeleo ya jamii pia kuepuka migogoro ya ardhi"

Pia kuna haja ya watendaji wapya kupata mafunzo elekezi ya namna ya ufanyaji kazi piaviongozi na watendaji a vijiji kufikisha ushiriki wa wananchi katika kupanga mipango ya bajeti.

Akielezea changamoto walizokutana nazo alisema kuwa baadhi ya viongozi wa vijiji  kufanya kazi kimazoea mfano kijiji cha Kilalakidewa .

Pia suala la ukubwa wa vijiji na vitongoji ni moja ya changamoto kubwa ya kutofikisha maendeleo kwa wakati kwa wananchi hivyo kuna haja ya kulitazama hilo.

Mtitu alisema suala la wanasiasa na wananchi kuingiza ajenda zao katika mikutano ya kimaendeleo ni moja ya sababu ya kukwamisha maendeleo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE