January 19, 2018

CHADEMA YAREJEA KWENYE CHAGUZI NDOGO ZIJAZO

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimempitisha Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Salum Mwalimu kugombea Ubunge jimbo la Kinondoni na Bwana Elvis Christopher Mosi kugombea jimbo la Siha. 
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema amesema hayo leo kuwa Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana jana jijini Dar es Salaam imefikia maamuzi hayo ya kushiriki kwenye uchaguzi mdogo kwenye majimbo ya Kinondoni na Siha unaotarajiwa kufanyika tarehe 19 Februari, 2018.
Mbali na hilo Mrema amesema kuwa wagombea wote wameshachukua fomu za uteuzi kutoka kwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo husika na watazirejesha kesho Jumamosi tarehe 20 Januari 2018 , kwa ajili ya uteuzi.
CHADEMA pamoja na UKAWA kwa ujumla na baadhi ya vyama vya upinzani nchini vilifanya maamuzi ya kutoshoriki katika uchaguzi mdogo wa marudio unaoendelea nchini kwa kile walichodai kuwa chaguzi hizo hazikuwa huru na haki na zilikuwa zimekiuka haki za binadamu kutokana na fujo na vurugu zilizokuwa zikifanywa katika chaguzi hizo. 
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE