January 15, 2018

CCM IRINGA YAFANYA KWELIMjumbe  wa  NEC  Taifa  Salim  Asas  akiwahutubia  wakazi  wa kata ya  Kihesa baada ya  diwani  wa CCM  kupita  bila  kupingwa
Mjumbe  wa  NEC  Taifa  Salim Asas  akimkabidhi kadi mmoja kati ya makada wa Chadema  waliojiunga na CCM


Diwani  mteule wa kata ya  Kihesa  Juli  Sawani Kushoto  akimshukuru Asas kwa  kumuunga mkono
Mjumbe  wa  NEC Taifa  Salim Asas  akimakabidhi kadi kada wa Chadema  aliyejiunga na CCM

Asas  akifurahia  jambo
Diwani  wa  Mshindo  Ibrahimu  Ngwada  akiwa na  diwani  mteule wa KItwiru  Baraka Kimata 
Diwani mteule wa kata ya Kihesa  Juli  Sawani  akivishwa taji
Diwani  wa Kihesa  Juli  Sawani  akipongezwa
Wana CCM na  wananchi Kihesa  wakifurahia
Mjumbe  wa  NEC Taifa  Salim  Asas  akimsikiliza kwa makini diwani mteule wa Kihesa  Juli  Sawani
Aliyekuwa katibu  mwenezi wa  Chadema kata ya  Kihesa akitangaza  kujiuzulu na kujiunga na CCM
Mwanahabari  Neema  Msafiri  akifuatilia  hotuba
Asas  akifurahia jambo na kada wa chadema aliyejiunga  CCM

KAZI ya  kupokea  jimbo la Iringa mjini  kutoka kwa mbunge wa chama  cha  Demokrasia na maendeleo (chadema) Mchungaji Peter Msigwa imeshika kasi baada ya  mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) anayewakilisha mkoa wa Iringa, Salim Asas kutangaza nnema kwa wananchi  wa Kihesa kama ahsante ya kumwezesha  diwani wa CCM Juli Sawani kupita bila kupingwa  katika uchaguzi mdogo .
Kwenye  hafla ya  kwanza  kupokea hati ya udiwani katika  viwanja vya Kihesa ,Asas aliahidi  ahadi  tatu za kimaendeleo kwa  kata ya  Kihesa  kubwa  ikiwa ni kuwawezesha  vijana kupata  ajira kwa  kuwezeshwa .
Katika  ahadi  zake  hizo ambazo utekelezaji  wake  utafanyika mapema  zaidi Asas alizitaja  kuwa ni  kumalizia ujenzi wa jengo la kitega uchumi la kata ya Kihesa linalojengwa pembeni mwa ofisi ya kata hiyo na kuchangia mifuko 200 ya sementi kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa madarasa mapya ya shule ya sekondari ya Kihesa.

Kwa kasi hii ni  wazi jimbo hilo mwaka 2020 CCM haitakuwa na kazi kubwa ya  kulikomboa toka kwa Chadema.
“Moja ya kazi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ni kusimamamia utekelezaji wa Ilani ya CCM. Ilani hii inazungumza maendeleo ya watu. Na kwa kuwa halmashuri zetu hazina mapato ya kushughulikia kero zake zote, zinahitaji ufadhili na michango ya kila mwenye nafasi,” alisema.
Alisema kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo.
Alisema vijembe na malumbano ya kisiasa katika kata hiyo yanatosha na akawataka vijana hao kuunda vikundi vya ujasiriamali vitakavyowawezesha kufikiwa kirahisi na mipango mbalimbali ya maendeleo.
Kwa upande wake diwani mteule wa kata hiyo aliahidi kutumia mfuko wake binafsi kukarabati barabara ya  Mafifi kwasababu imekuwa kero kubwa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo.
“Kazi hii itaanza wiki hii na sio kwa kutumia greda la manispaa, hapana, nitatufuta greda lingine kwa gharama zangu na litaifanya kazi hiyo kuanzia wiki hii,” alisema.
Sawani alizungumzia pia namna wananchi wa kata hiyo wanavyotakiwa kujiondoa na umasikini kwa kufanya kazi yoyote halali na kwa bidii huku akiasa kwamba hakuna kiongozi wa kisiasa wakiwemo madiwani wanaochaguliwa kwa lengo la kugawa fedha kwa wananchi.
“Kuweni na ndoto za kuondokana na umasikini na zitumie ndoto hizo kuja na mikakati na mipango itakayowaondoka katika hatua moja kwenda nyingine ya mafanikio,” alisema.
Sawani aliwashukuru wana CCM, wananchi wa kata hiyo na vyama vingine vya siasa ambavyo kwa heshima yake alisema havikusimamisha wagombea na kumfanya apitwe bila kupingwa.
“Kwa heshima hiyo najiona nina deni kubwa sana kwa wananchi wa kata hii, niombe ushirikiano kutoka kwenu kwasababu mchakato wa maendeleo unaohusisha nguvu zetu wote,” alisema.

Katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali, wabunge na wapenzi wa chama hicho, Asas aliwapokea wanachama wapya 53 kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuwakabidhi kadi za chama chake.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE