January 17, 2018

BREAKING NEWS:WATU WASIOJULIKANA WATEKETEZA NYUMBA YA KATIBU UVCCM IRINGA MJINI

Nyumba  aliyokuwa  akiishi  katibu wa UVCCM Iringa mjini Patrick Muyinga iliyochomwa  moto na  watu wasiojulikana
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela na mkuu  wa mkoa Amina Masenza wakitazama  chumba ambacho alikuwa akiishi katibu  wa UVCCM wilaya ya  Iringa mjini  kilivyoteketea kwa  moto
Wanafunzi  waliokuwa  wakiishi katika  nyumba  hiyo wakiwasili  kutoka Hoteli  walikolala  leo
Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa  Richard Kasesela  na  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza wakiwa  eneo la  tukio
Chumba  cha katibu  wa UVCCM wilaya ya  Iringa mjini  kilichoteketea  kwa moto baada  ya  wasiojulikana  kuchoma  moto nyumba
Na MatukiodaimaBlog
WATU  wasiojulikana waliovunja  nyumba  ya   diwani wa Kata ya Mwangata Jimbo la Iringa mjini  aliyejiuzulu Chadema ,wameiteketeza kwa moto nyumba  aliyekuwa akiishi katibu ya  umoja  wa  vijana wa chama  cha mapinduzi (UVCCM)  wilaya ya  Iringa mjini Patrick Muyinga yachomwa  moto.

Nyumba hiyo  ipo eneo la Njiapanda ya Beda  kata  ya  Kihesa  imechomwa   usiku  wa  kuamkia  leo  baada ya  watu hao  kuvunja  dirisha ya  chumba  cha katibu  huyo na  kurushia kitu chenye  mlipuko .

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Amina Masenza akizunguzia  tukio  hilo la  lile la diwani  kuvunjiwa  nyumba  alisema  kuwa ni matukio ambayo  yanahusishwa na  visa  vya  kisiasa na  kumtaka  kamanda wa  polisi  mkoa  wa Iringa  Julius Mjengi  kuwasaka  wote  wanaohusika na matukio  hayo .
Katika  tukio hilo hakuna  aliyepoteza maisha wote  wametoka  salama  ila mali  zote  zimeungua moto .

Habari  kamili  soma  gazeti la Mtanzania Kesho

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE