January 17, 2018

BREAKING NEWS AJALI YAUA IRINGA

Wakazi wa Tanangozi wilaya ya Iringa mkoani Iringa wakitazama ajali ya lori moja kufeli breki na kugonga malori mengine manne yaliyokuwa yameegeshwa eneo hilo  na kusababisha kifo cha mtu usiku wa kuamkia leo
r="1" style=
Mtu mmoja amepota maisha baada ya Lori lenye namba  T508DEC likiwa tela T204DE likitokea nchini Zambia kuelekea Dar es Salaam  kufeli breki na kuyagonga malori manne yaliyokuwa yamepaki eneo la Tanangozi wilaya ya Iringa mkoani Iringa .

Mwandishi wa Matukio daima  Tanangozi  Brayson Mpwepwa amehabarisha kuwa ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia Leo katika eneo la mji wa Tanangozi kwenye Barbara kuu ya Mbeya -Iringa.

Alisema kuwa katika ajali hiyo mtu mmoja ambae ni utingo wa lori hilo amepoteza maisha papo huku dereva wa Lori akitolewaakiwa mahututi.

Jeshi la polisi wapi njiani kuelekea eneo la tukio habari zaidi tutaendelea kuwajuza ikiwa ni pamoja na kumtafuta kamanda wa polisi Mkoa wa Iringa Julius Mjengi.

Video za tukio hili zitakujia hivi punde katika Chanel ya YouTube ya matukiodaima tembelea sasa kisha usisahau kujiunga kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa Subscriber

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE