January 30, 2018

AFRIKA YAAZIMIA KUZALISHA UMEME WA KUTOSHA-MAJALIWA


Waziri Mkuu Kassima Majaliwa amesema nchi za Bara la Afrika zimeazimia kujiimarisha katika uzalishaji wa umeme hadi vijijini ili uweze kuleta maendeleo.
Waziri Mkuu Kassima Majaliwa.
Waziri Majaliwa ameeleza hayo wakati alipokuwa anazungumza baada ya mkutano wa viongozi wa wakuu wa Nchi za Afrika uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia ambapo alimuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli na kusema nchi za Afrika zimejipanga kuzalisha umeme wa kutosha mijini na vijijini.
Waziri Mkuu alisema nchi hizo zimeazimia kuzalisha umeme mwingi kwa lengo la kuinua kiwango cha maisha ya wananchi wake na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.
"Nchi za Afrika zinatakiwa zijitegemee kiuchumi, ambapo nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya nyingine za Afrika zimefikia mapendekezo ya kuimarisha uzalishaji wa umeme. Tanzania iko vizuri kwa sababu ina vyanzo vingi vya kuzalisha umeme na sasa ina mikakati ya kuzalisha umeme wa kutosha kuendesha viwanda vikubwa na kukaribisha wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali", alisema Majaliwa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema maelengo ya mkutamo huo yalikuwa ni kupokea taarifa za tume mbalimbali zilizoundwa katika kikao kilichopita ambapo ni pamoja na tume iliyokuwa inashughulikia masuala ya usalama na amani katika Bara la Afrika.
"Tume nyingine ilihusika na mapitio ya namna kuhamasisha nchi za Afrika kufikia kwenye maendeleo na nyingine ilikuwa inahamasisha mahusiano ya nchi kupitia kwenye Jumuia zilizopo ndani ya Bara la Afrika kama SADC", alisisitiza Majaliwa.
Pia Waziri Mkuu alisema mkutano huo ulifanya mapitio ya mapendekezo ya namna nchi za Afrika zinavyoweza kupata mitaji kupitia michango ya nchi mbalimbali, ambapo  kanuni ziliandaliwa ili kuwezesha kila nchi kuchangia katika mfuko mkuu wa Umoja wa Afrika.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE