January 1, 2018

AFGHANISTAN: WATU 17 WAUAWA KWENYE SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA

Image result for AFGHANISTAN: WATU 17 WAUAWA KWENYE SHAMBULIO LA KUJITOA MHANGA
Watu 17 wameuawa baada ya mtu mmoja kujiripua mhanga kwenye mazishi katika wilaya ya Behsud katika jimbo la Nangarhar lililopo mashariki mwa Afghanistan.
Mshambuliaji huyo alijiripua wakati wa mazishi ya aliyekuwa gavana wa jimbo hilo aliyefariki kifo cha kawaida.
 Mkurugenzi wa afya wa mkoa Najib Kamawal ameeleza kuwa watu wengine 14 wamajeruhiwa.
Hakuna mtu au kundi lililodai kuhusika na shambulizi hilo ingawa makundi ya Taliban na lile linalojiita Dola la Kiislamu yamezidisha mashambulizi katika miezi ya hivi karibuni.
Picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha vidimbwi vya damu, nguo na viatu vilivyozagaa.
Shambulizi hili limetokea siku chache baada ya kundi la IS kudai kuhusika na shambulizi katika kituo cha utamaduni cha Washia ambapo watu 41 waliuawa na wengine zaidi ya 80 walijeruhiwa.


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE