December 7, 2017

WENYE UKIMWI WANAOKWEPA DAWA MRADI WA SAUTI YETU KUWAFIKIA

MTAKAKATI  wa  kuwasaidia  waathirika  wa  virusi  vya  UKIMWI wanaokwepa kutumia  dawa  umezinduliwa  mkoani  Iringa  ili  kuwawezesha wale  wote  wanaokwepa  dawa  kuendelea  kutumia  dawa  za  RAVS.

Wakizungumzia  juu ya harakati  hizo leo   wakati  wa  uzinduzi  wa  mradi  wa  SAUTI  YETU katika Halmashauri  ya  Iringa vijijini  wadau  wa  mradi  huo  walisema  kuwa kuanzishwa  kwa  mkakati  huo ni  hatua  kubwa  ambayo  itasaidia  kuwawezesha watu  hao  wanaoishi na  VVU  kuendelea  kutumia  dawa .

Makamu  mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Iringa Rita Mlagala akizungumzia mkakati  huo  alisema moja  kati  ya  mikakati itakayowezesha  watu  wenye  VVU  kuweza  kutumia  dawa  bila  kuacha  ni pamoja  na kuendelea  kuhamasishwa  kama  ambayo  mradi  huo wa  SAUTI  YETU  ulivyoanza  katika  Halmashauri  hiyo .

Alisema  kuwa  kati  ya  maeneo  ambayo  yapo  kwenye  changamoto  ya  maambukizi  ya  VVU  na  hofu  ya  walengwa  kutotumia  dawa  ni  pamoja na  kata ya Malenga makali ambako  kuna  machimbo ya  madini hivyo  kuwepo  kwenye  mradi huo  kutawezesha  walengwa  kujitambua na  kupata dawa  bila  kuacha.

Mratibu  wa  mradi  wa  SAUTI  YETU kanda  ya  Mbeya Humphrey Leonard  alisema  kuwa   katika  kuongeza jitihada  za  muitikio  wa  UKIMWI kwenye  mikoa  ya  Iringa  baraza  la  Taifa  la watu  wanaoishi  na  Virusi  vya  UKIMWI  Tanzania  (NACOPHA)kupitia ufadhili  wa  watu  wa  Marekani (USAID)  wametekeleza mradi  wa  SAUTI YETU katika mikoa 21 na  Halmashauri  46 Tanzania  bara .

“ Mradi huu  ulianza   kutekelezwa Disemba mwaka 2013 na  kutarajiwa kumalizika mwaka  2019  kupitia mradi  wa  SAUTI  YETU baraza  limeezesha juhudi  za  watu wanaoishi na VVU (WAVIU)  kupitia mabaraza  yake ya  Halmashauri (KONGA)  kupata fursa  ya kutekeleza mradi huu  ndani ya  Halmashauri 29 hadi sasa”

Alisema  kuwa  mradi huo  umelenga  kutoa fursa kwa WAVIU  kushiriki  moja  kwa  moja  katika utekelezaji wa  huduma za  UKIMWI kwenye jamii  na kuhakikisha  lengo  la kufikia mkakati wa  90-90-90 unafikiwa  kwa  kuhakikisha asilimia 90 ya wanajamii katika  maeneo ambayo mradi unatekelezwa wanakwenda  kupima na kutambua afya  zao  juu ya maambukizi ya  VVU na  kuhakikisha  asilimia 90 walioambukizwa VVU wanaanzishiwa huduma ya  tiba  na  kudumu kwenye  tiba.

Leonard alisema  katika  Halmashauri   ya  Iringa  vijijini  mradi huo  utafanya kazi kwenye  kata tano  ambazo  ni  Mlenga, Kising’a,Malenga  Makali , Kihorogota  na Lyamugungwe  na  kuwa  wanufaika  wa msingi  wa mradi  huo   watakuwa ni  watu wote wanaoishi na VVU,wanajamii, na  asasi za  kiraia zilizo katika muitikio  wa  UKIMWI pamoja na  watunga sera katika ngazi mbali  mbali .


 Afisa  tathimini  na ufuatiliaji  wa  mradi  huo Ally  Mamlo  alisema  kuwa  kumekuwepo  na mafaniko  makubwa  katika  baadhi ya  maeneo  ambayo  mradi  huo unatekelezwa na  kuwa katika  Tanazania  Bara mradi   huo  unatekelezwa  mikoa 21  ambayo ni  Shinyanga, Morogoro, Njombe  , Simiyu, Geita,Dodoma,Iringa , Songwe ,Mwanza , Mbeya, Mara, Rukwa , Dar  es  Salaam , Lindi ,Tanga, Mtwara ,Arusha ,  Kilimanjaro ,Tabora  na Kigoma.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE