December 29, 2017

WAZIRI MKUU WA UHISPANIA ATAKA KUUNDWA KWA BUNGE LA CATALONIA

Image result for Waziri Mkuu wa Uhispania ataka kuundwa kwa bunge la Catalonia 2017
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy ametoa wito wa kuundwa kwa bunge la Catalonia ifikapo Januari 17 mwakani, ikiwa ni hatua ya kwanza ya kurejesha serikali ya mkoa iliyokuwa imevunjwa na Madrid baada ya kujitangazia uhuru kinyume na sheria mwezi Oktoba.

 Mara ya baada ya bunge kuzinduliwa, wabunge watakuwa na kibarua cha kuteua mgombea wa kuiongoza serikali na ambaye atapigiwa kura ya kuwa na imani naye.

Vyama vinayopigania kujitenga vilijinyakulia ushindi mwembamba katika uchaguzi wa Desemba 21, lakini wanaweza kupata ugumu katika kuunda serikali wakati wengi wa viongozi wake wakikabiliwa na kesi za kisheria kuhusiana na ushiriki wao katika harakati za kujitangazia uhuru.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE