December 14, 2017

WATUMISHI 1000 NA JAMAA ZAO KUBANWA NA TUME YA MAADILI

ZAIDI  ya  viongozi  1000  kuhojiwa na  sekretarieti  ya  maadili  ya  viongozi  wa  umma  kanda  ya  nyanda  za juu  kusini Mbeya  pamoja  na ndugu  zao  wa karibu  ambao  wana  mali zilizonje  ya  uwezo  wa  kipato  chao.
Mbali  ya  kuwahoji  hao  pia  watumishi  wa  umma  ambao kila  mwezi   hutoka  patupu  bila  kupokea  chochote  katika  mishahala  yao  kutokana na madeni  mengi nao  kufikishwa  katika tume ya  maadili ya  utumishi  wa  umma  kujieleza  namna  wanavyoweza  kuishi  bila  kulipwa  mishahara mwisho  wa  mwezi.
Akizungumza  katika  maaadhimisho ya  siku ya maadili  mkoa  wa Irina  iliyofanyika  kwenye  ukumbi  wa  Siasa  ni  kilimo  mjini  Iringa juzi mkuu wa  kanda  wa sekretarieti  ya  maadili ya  viongozi  wa  umma kanda ya  nyanda za  juu  kusini , Erick Mbembati alisema  utaratibu  wa  kuwahoji  viongozi  wa  umma na  uhakiki  wa  mali  zao  umekuwa  ukifanyika .
Alisema  jumla ya  viongozi  500 wamekwisha  hojiwa  kuhusiana  na maadili  na  sasa  ni  zamu ya  viongozi  zaidi ya  1000 kuwa   wapo  baadhi ya  viongozi  ambao  wamekuwa hawatoi taarifa  za  kweli  hivyo  kutokana na  hali  hiyo  wamekuwa na  kuzifanyia  uhakiki  taarifa   hizo  kwa  kuzifanyia  uchunguzi  zaidi  ili  kujua  ukweli  wa  taarifa  wanazotoa  watumishi  wa  umma.
Hata  hivyo  alisema  baada ya  Rais  kusaini  mabadiliko  ya  sheria   hiyo  hivi  sasa  wanaouwezo  wa  kumuita  kiongozi  yeyote  kwa  hati  maalum na  kufika katika  tume  ya  maadili ya  kuhojiwa  kwa  gharama  zake .
“ Kuna  mchakato  wa  kuandaa sheria  ya  mgongamo  wa  kimaslahi ambayo  iwapo  itaridhiwa na  wabunge basi  itasaidia  zaidi  kuweza kufanya  kazi   hiyo ya  uhakiki  wa mali  za  watumishi  wa  umma  bila  kuwepo  kwa  chembe  ya mgongano wa kimaslahi tatizo  kubwa  lililopo  sasa  ni  mgongano wa  kimshali  ya  mtu  binafsi na maslahi  ya umma  kwa  kuacha  yale ya  umma  na  kutimiza  maslahi  binafsi “
Mbembati  alisema  kuwa mara  baada ya  kukaa wale  watakaokutwa na makosa hupelekwa  kwenye  baraza la maadili ya  watumishi  wa  umma  pia  alisema  katika  sheria   hiyo  iliyosainiwa na  Rais  tarehe 7 /7 /2016  inawapa  nafasi  ya  kuwabana  rafiki na  ndugu  wa karibu  kwa  mali  wanazomiliki ama  mihamala  ya  kifedha  imnayopitishwa  kwa  rafiki  wa  jirani .
Kwa upande wake  mkuu wa  mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza aliwataka  watumishi  wa  umma  kuweza  kujitambua  ili kuelekea  katika uchumi  wa  kati na  kuwa maaadhimisho hayo  katika  mkoa  wa  Iringa yalibebwa na kauli mbiu isemayo  wajibika  piga  vita  rushwa ,zingatia maadili ,haki  na  utawala  bora kuelekea  uchumi  wa  kati  ni  vema  kila  mmoja  kuzingatia  na  pale  ambapo  walijikwaa  basi  kujirekebisha
  Rais  wetu  Dkt  John  Magufuli   amekuwa mbele  katika  mapambano ya  rushwa na  kuona  Taifa   linapiga  hatua  katika  Nyanja  mbali  mbali  ikiwemo  ya  viwanda hivyo kwa  pamoja   hatuna  budi  kuungana  kutekeleza majukumu  yetu  na  kufanya  kazi  na  kujiepusha  na  Rushwa  pamoja  na  maadili  yasiyofaa kwa  watumishi  wa  umma”
Mkuu   huyo  wa  mkoa  pia aliwaomba  viongozi  wa  dini  kutumia  nafasi  zao  kutoa  elimu  kwa  waumini  wao  dhidi ya  Rushwa  pamoja  na  ukuzaji  wa  uchumi  kwa  mtu mmoja  mmoja   pamoja na  kuwajenga  vijana  katika  uadilifu  ili  kukuza  uchumi  wa  viwanda  na  kuwaepusha   vijana  na  ulevi  uliopindukia.
Mwakilishi  wa Kanisa  la  kiinjili  la  Kilutheri Tanzania  (KKKT)  Iringa , Emma  Mwalusamba alisema  kuwa  changamoto  ya  maisha  ya  sasa  ni  watu  wengi  kutokuwa na  hofu ya  Mungu  na  ndio  sababu ya  mambo  kwenda  ndivyo  sivyo .
Alisema  kuwa  suala la  maadili  kwa  jamii  linaendelea  kumomonyoka  siku  hadi  siku  kutokana na  watu   kukosa  hofu ya  Mungu  na  kukosa  upendo miongoni  mwao  hivyo  kuna haja  ya  kila  kiongozi  na  kila  mmoja  kujitathimini  katika  utendaji kazi  kuepuka  kuomba  rushwa  kwa  wale  wanaohitaji   huduma.
Kamanda  wa Taasisi ya  kuzuia na kupambana na  Rushwa  (TAKUKURU)  mkoa wa  Iringa Aidan Ndomba  akitoa  mada  juu ya Rushwa alisema   kuwa  rushwa   inatokea  pale  ambapo  mtu mwenye kuhodhi  madaraka anatumia  uwezo  wa  kuamua jambo  kwa  vile anayo sheria ,kanuni  inayompa mamlaka lakini  hufanya   hivyo  pasipo  kuweka  wazi  sababu  za  kutoa uamuzi huo  wala kuwa  tayari  kuelezea sababu  za  kufanya   hivyo .

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE