December 15, 2017

WATEJA WA TANESCO KANDA YA DAR ES SALAAM NA PWANI SASA WANAWEZA KULIPA BILI KUPITIA BENKI YA NMB

 

WATEJA wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ambao hawatumii mita za LUKU, sasa wanaweza kulipia bili zao za kila mwenzi kupitia benki ya NMB, na huduma hiyo inaanza kwa majaribio Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za TANESCO Mikocheni jijini Dar es Salaam Desemba 15, 2017, Meneja Masoko wa Tanesco, Mussa Chowo amesema, huduma hiyo ni kuwarahisishia wateja kuondokana na usumbufu wa kuzifikia ofisi za TANESCO kufanya malipo hayo na badala yake wanaweza kutumia benki ya NMB kufanya malipo.


“Tunaanza kwa majaribio katika kanda ya Dar es Salaam na Pwani na tukiona inakwenda vizuri tutapanua huduma hii kwenye mikoa mingine.” Alisema. Pichani Bw.Chowo (kulia), akitoa taarifa hiyo leo Desemba 15, 2017 jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja Tehama, Utafiti na utengenezaji mifumo, Evaristo Winyasi.

 NA K-VIS BLOG


0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE