December 25, 2017

Wanasayansi wapata picha za nguruwe wenye sura mbaya zaidi duniani

     

Javan warty pig captured on a camera trap Wanasayansi wapata picha za nguruwe mweye sura mbaya zaidi duniani                
Wanasayansi wamepata picha za kwanza za msituni za kati ya nguruwe wachache wenye sura mbaya zaidi duniani.
 
Kamera fiche kwa sasa zimefichua kuwa idadi ndogo wa nguruwe hao bado wanaishi maeneo ya misitu kadha huko Java.
Wanasayansi wanasema kuwa lengo lao ni kulinda makazi ya wanyama hao.
Camera trap attached to a tree
  Kamera fiche kwa sasa zimefichua kuwa idadi ndogo wa nguruwe hao bado wanaishi maeneo ya misitu kadha huko Java.                
Mkuu wa utafiti huo Dr Johanna Rode-Margono, alisema kuwa wanasayansi walifurahishwa kugundua kuwa nguruwe hao bado wako.
Utafiti wa mwisho kwenye misitu hiyo ulifanywa mwaka 2004 na kuonyesha kuwa idadi ya nguruwe hao ilikuwa ikididimia zaidi.
 
"Tuliogopa kuwa wote au wengi zaid walikuwa wametoweka," aliiambia BBC.
Kati ya maeneo saba ambayo wanasayansi waliyafanyia uchunguzi wakitumia kamera fiche, ni matatu tu yaligunduliwa kuwa na nguruwe hao.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE