December 4, 2017

WAHITIMU CHUO KIKUU IRINGA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI

pIC 1
Wahitimu  wa Chuo Kikuu cha Iringa wakipita mbele ya Mkuu wa Chuo Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani kwa ajili ya kutunukiwa vyeti vyao katika maadhimisho ya mahafali ya 20 ya chuo hicho siku ya Jumamosi Mkoani Iringa.
PIC 2
Wahitimu wa Shahada ya Sheria (LL.B) katika chuo Kikuu cha Iringa wa kwanza kulia Richard Kipingu, Charlotte A. Mwaigwisya(wa pili kulia) ,Msumi Shabani(katikati),Catherine Eliwako Mjemah(wa pili kushoto) na Edwin Mushi(wa kwanza kulia)  wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maadhimisho ya  mahafali ya 20 tangu kuanzishwa kwa chuo hicho siku ya jumamosi Mkoani Iringa
Picha na Mpiga picha wetu.
……………..
Na Mwandishi Wetu Iringa
Mkuu wa Chuo Kikuu Iringa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani amewataka wahitimu wa chuo hicho kufanyia kazi yale yote waliyojifunza darasani kwa kuzingatia maadili ili kujenga taifa bora.
Akizungumza katika mahafali ya 20 ya Chuo hicho siku ya jumamosi MKoani Iringa Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani alieleza kuwa taifa bora hujengwa kwa kuzingatia maadili mema.
“Taifa bora hujengwa kwa kuzingatii maadili mema ambayo ni utii,heshima,kufuata sheria,kanuni na taratibu za utendaji kazi kwa jamii husika “ alisema Jaji Mkuu Mstaafu Ramadhani.
Aidha aliongeza kwa kuwataka wanafunzi hao kuunga mkono juhudi za Seriklai ya awamu ya Tano chini ya Uongozi wa Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli katika kuhakikisha tunafikia uchumi wa viwanda.
Naye Mhadhiri katika Kitivo cha Sheria wa Chuo Hicho Bw. Renatus Mgongo amewahisi wahitimu hao kuwa waadilifu katika utekelezaji wao wa majukumu ili kuleta matokeo chanya kwa Taifa.
Katika mahafali hayo wahitimu waliotunukiwa vyeti katika ngazi mbalimbali ikiwa ni pamoja na shahada ya Uandishi wa  Habari (35), Shahada ya Theolojia-Divinity (9), Shahada ya Sheria (172), Shahada ya Utawala wa Biashara (110), Shahada ya Elimu Katika Hisabati (82 na  Shahada ya Ushauri Nasihi (58),
Wahitimu wengine walitunukiwa Shahada ya Maendeleo ya Jamii (205), shahada ya Sayansi ya Technolojia ya Habari-IT (30) na Shahada ya Athropolojia ya Utamaduni na Utalii (139),
 stashahada ya Theolojia (14), Cheti cha Utawala wa Biashara (88), Cheti cha Theolojia (12) na Cheti cha Sheria (6).

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE