December 13, 2017

MGOBASA COLOUR LAB YAANZA KUKUZA UTALII MIKOA YA KUSINI

Baadhi  ya wanahabari  mikoa ya  kusini  na  wadau  wa  utalii wakiwa  mbioni  kutembelea hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha  mkoani Iringa kuhamasisha  utalii  wa  ndani kama  shabaha ya  serikali  kufungua  lango  la  utalii  kusini ,waandishi hawa na wadau  hao  ziara  yao  ilifadhiliwa na studio  ya kisasa  Njombe ya Mgobasa
Wanahabari  na  wadau  wa  utalii  wakiwa  njiani  kuelekea  hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha 
 
Utalii  wa  ndani chini ya  ufadhili wa Mgobasa
Hali  ya  viboko hifadhi ya  Ruaha
KATIKA  kuhamasisha  utalii  wa  ndani na ukuzaji  wa  sekta ya  Utalii Mgobasa Photo Studio  imeendelea  kuunga  mkono  jitihada za  serikali ya  awamu ya  tano  katika  ufunguaji  wa lango  la  Utalii mikoa ya  kusini  maarufu kama  karibu  kusini  kwa  kudhamini wadau  wa  sekta ya  utalii  wakiwemo  wanahabari kutembelea hifadhi ya  Taifa ya  Ruaha .

Mgobasa kupitia  hamasa  kubwa  aliyoifanya  kupitia  vyombo  vya  habari kwa  muda ameweza  kuwawezesha wadau  wa  sekta ya  utalii mkoa  wa Njombe wakiwemo  wanahabari kutembelea  hifadhi  hiyo ya  taifa kujifunza na  kuhamasisha utalii  wa  ndani .


Tangazo hilo ambalo limekuwa likitangazwa katika vyombo mbalimbali vya habari vilivyoko mkoa wa njombe na Iringa liliwataka wapigapicha anaosafisha picha katika studio za mgobasa zilizoko wilaya ya mbarali Mbeya,Njombe,makambako na Songea mkoani Ruvuma kushindania kinyanganyiro cha kupata fursa ya kufanya utalii wa ndani.

Mapema saa kumi na mbili nje ya ofisi ya Mgobasa makambako ya kusafisha picha wapigapicha Zaidi ya 40 wanaanza safari kuelekea ruaha national park kilomita Zaidi ya 85 kutoka kitovu cha mji wa Iringa.

Baada ya kuwasili getini kwanza ni kujiandikisha na kisha kupewa maelekezo kupitia maafisa utalii [tour guides]

Baada ya mwendo kidogo kila mmoja anahuzunika kuona Wanyama wanaoisi majini wakiwemomaba na viboko kuishi katika maji yenyekina kifupi na kuonekana wakiteseka,ambapo waliowengi wanahoji maafisa utalii ni kwaninini maji yamepungua na namna ya kutatua tatizo,licha ya majibu kutopatikana kwa haraka.

Aidha katika ziara hiyo ya utalii iliyojumuisha wapiga picha kutoka njombe mjini , makambako,Rujewa,na songea pamoja na waandishi wa habari itv,clouds media na kings fm radio,afisa utamaduni makambako na walimu wawili wa shule za msingi makambako zilizofanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mjini makambako ambazo sigridi na azimio,
Imewafanya washiriki kufanikiwa kuwaona Wanyama kama twiga,tembo,swala,kiboko,mamba,kanga,simba,na pundamilia kwa siku ya kwanza na kuwafanya kufurahi saana

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE