December 16, 2017

USAJILI DIRISHA DOGO KURUDIWA TENA -TFF
Kipindi cha dirisha dogo la usajili kwa vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza Tanzania Bara kilichomalizika jana Desemba 15, 2017 huenda kikaongezewa muda kutokana na matatizo yalioukumba mfumo wa usajili wa shirikisho la soka duniani (FIFA). 

Akizungumza na UFM jioni ya leo, afisa habari wa TFF, Alfred Lucas (pichani) amesema mfumo wa FIFA unaosimamia zoezi la usajili kwa wanachama wake umekumbwa na matatizo ya kiufundi ambayo bado yanashughulikiwa hivyo huenda Tanzania ikapewa muda wa ziada kwa vilabu vyake kufanya usajili. 

"Mfumo wa usajili wa FIFA ume ‘collapse’ hivyo kuna matatizo ya kiufundi yanaendelea kushughulikiwa na mafundi wa FIFA huko Uswisi, mfumo ukishakuwa tayari basi Tanzania watapewa muda wa ziada wa saa 24 tangu kurudi kwa mawasiliano hayo”. Amesema Lucas kupitia 107.3 UFM

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE