December 26, 2017

UMOJA WA ULAYA WAKOSOA URUSI KUMZUIA NAVALNY KUWANIA URAIS MWAKANI

Umoja wa Ulaya hii leo Jumanne umeshutumu uamuzi wa maafisa wa Urusi wa kumzuia mwanasiasa wa upinzani Alexei Navalny kuwania urais katika uchaguzi utakaofanyika Machi 2018.
 Kwa mujibu wa taarifa ya kitengo kinachohusika na masuala ya nje katika Umoja wa Ulaya , hatua hiyo inaonesha mashaka iwapo uchaguzi huo wa mwakani utafanyika kwa kufuata misingi ya kidemokasia.
 Tume ya uchaguzi nchini Urusi jana Jumatatu ilitangaza kumzuia Navalny kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi wa mwakani ikimhusisha na mashitaka ya ubadhirifu. 
Hata hivyo Navalny ambaye pia ni mwanasheria anasisitiza mashitaka dhidi yake yamechochewa kisiasa. 
Umoja wa Ulaya umesema mashitaka yanayochochewa kisiasa hahapaswi kutumika dhidi ya haki ya mtu kushiriki siasa.
 Wakati huohuo Ikulu ya Urusi Kremlin hii leo imepuuza juu ya wasiwasi uliopo kuhusiana na uamuzi wa kumzuia Navalny kushindana na rais Vladimir Putin katika uchaguzi wa mwakani kuwa inaondoa uhalali wa uchaguzi huo.
 Msemaji wa Kremlin Dmitry Pescov amesema hawakubaliani na kauli hiyo na kusisitiza kuwa kauli yoyote ya kususia uchaguzi inapaswa kufikiriwa kwa umakini.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE