December 31, 2017

UJERUMANI YAINGIA MWAKA 2018 BILA SERIKALI MPYA

Kansela wa Ujerumani mhafidhina Angela Merkel anayekabiliwa na shinikizo kufuatia hadi sasa kushindwa kuunda serikali mpya ya muungano ikiwa ni miezi mitatu baada ya kufanyika uchaguzi mkuu, leo Jumapili aliapa kushughulikia changamoto zinazosababisha kuongezeka mgawanyiko katika jamii mnamo wakati akipigania kunda serikali iliyo thabiti.
 Katika hotuba yake ya kuukaribisha mwaka mpya Kansela Merkel alianisha vipaumbele kadhaa vya msingi ikiwa ni pamoja na kuongeza uwekezaji katika masuala ya ulinzi na usalama, kuboresha huduma za afya na elimu.
 Merkel anayekabiliwa na shinikizo la kuunda serikali mpya anajaribu kukishawishi chama cha Social Democratic SPD kukubali kuunda serikali mpya ya muungano kama ilivyokuwa miaka minne iliyopita licha ya vyama vyote hivyo viwili kutopata matokeo ya kuridhisha katika uchaguzi wa Septemba.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE