December 6, 2017

UFUNGUZI WA ZOEZI USHIRIKIANO IMARA 2017 WA JWTZ


Wito wa Vyombo vya Habari


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa kuwa litafanya zoezi la kijeshi litakalojumuisha majeshi ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki lijulikanalo kama “Ushirikiano Imara“ 2017. Zoezi hilo litafunguliwa rasmi kesho tarehe 07 Desemba 2017 saa 3:00 Asubuhi katika viwanja vya Chuo cha Ulinzi wa Amani (PTC) Kunduchi jijini Dar es Salaam.  Mgeni rasmi kwenye ufunguzi huo ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Dkt. Hussein Mwinyi.
JWTZ linapenda kukialika chombo chako cha Habari katika sherehe za Ufunguzi wa zoezi hilo.


Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
06 Desemba, 2017.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE