December 4, 2017

STARS ILIVYOANZA NA SARE MICHUANO YA CECAFA

IMG-20171203-WA0053
Timu ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ imeanza sare ya bila kufungana na wabuguzi wa rangi Libya katika mchezo wa Kundi A wa Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati ‘CECAFA Challenge Cup’ mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Machakos nchini Kenya
IMG-20171203-WA0052
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Alex Muhabi aliyesaidiwa na Okelo Dick wote wa Uganda na Kakunze Herve wa Burundi, Libya ndio waliotawala zaidi na kutengeneza nafasi nyingi, lakini bahati mbaya umaliziaji ukawaangusha.
Tanzania Bara, au Kilimanjaro Stars ya kocha Ammy Ninje haikucheza kwa muunganiko wa kitimu zaidi kila mchezaji alicheza kivyake.
IMG-20171203-WA0048
Mbaya zaidi sehemu ya kiungo ilizidiwa na haikuwa na ubunifu kabisa, hivyo kuwapa nafasi Libya kutawala.
Angalau baada ya kuingia Jonas Mkude, sehemu ya kiungo ya Kilimanjaro Stars ilianza kucheza vizuri na hapo ndipo walipoanza kufika kwenye eneo la wapinzani na kupeleka mashambulizi kadhaa. 
IMG-20171203-WA0049
Katika mchezo wa kwanza wa Kundi A na mashindano kwa ujumla, wenyeji Kenya waliichapa Rwanda 2-0 Uwanja wa Bukhungu, Kakamega, mabao ya Masoud Juma kwa penalti na Otieno Duncan.  Amavubi ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya Kayumba Soter kutolewa kwa kadi nyekundu.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja ya Kundi B, Uganda wakimenyana na Burundi Kakamega kuanzia Saa 9:00 Alasiri.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE