December 29, 2017

SERIKALI KUJENGA MTAMBO WA KUZALISHA UMEME WA MAJI MTO RUFIJI

Image result for Serikali Kujenga Mtambo Wa Kuzalisha Umeme Wa Maji Mto Rufiji
Serikali inatarajia kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme  wa maji wa mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji ambao utasaidia kuimalisha  miundombinu ya umeme na upatikanaji wa uhakika kwa wananchi.

Akizungumza wakati wa ziara ya siku moja ya  kikazi Wilayani Chato Mkoani Geita iliyokuwa na lengo la kukagua na kujionea miundombinu ya umeme wa Rea  awamu ya tatu ,Waziri wa Nishati ,Dr Medadi Kalemani ,alisema kuwa hali ya umeme inaendelea kuimarika siku hadi siku na kuna maeneo mengi yameanza kupata umeme wa kutosha.

“Hapo Nyuma mwezi Novemba tulikuwa tunajitahidi kukarabati mahali ambapo kulikuwa na ubovu wa mitambo lakini kwa sasa hali inaendelea vizuri maeneo mengi ya nchi yetu yanapata umeme kwa wingi  na  tunaanza kujenga mradi mpya wa kuzalisha umeme wa maji wa  mega watt 2100 kwenye maporomoko ya mto Rufiji  ambao utasaidia kuimalisha  miundo mbinu ya umeme na upatikanaji wa umeme hapa nchini”Alisema Kalemani.

Aidha Dr,Kaleman  amewasisitiza wananchi kutoa taarifa kwenye maeneo yao pindi kunapotoakea tatizo na kwamba wateja ambao wamelipia umeme kwa mwaka 2017 ni vyema Tanesco wakahakikisha wanawaunganishia umeme haraka iwezekanavyo kwani mwaka 2018 haitakiwi kuwepo kwa mteja ambaye ajaunganishiwa  huduma hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE