December 2, 2017

OLE SOSOPI MWENYEKITI MPYA WA CHADEMA-VIJANA

Baraza la vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) limeteua mwenyekiti mpya baada ya Patrobas Katambi aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Baraza hilo limemteua aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Bara, Patrick Ole Sosopi kuwa Mwenyekiti mpya wa BAVICHA taifa kuchukua nafasi ya Patrobas Katambi aliyehamia CCM.
Aidha Baraza hilo limemteua ndugu John Pambalu kuwa katibu wa BAVICHA baada ya nafasi hiyo kuachwa wazi na Ole Sosopi aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa muda wa BAVICHA taifa.

Kabla ya maamuzi na uteuzi huo kufanyika, Baraza la Uongozi la Chama hicho lilikutana jana na kujadili mwenendo wa chama hicho, kuweka mikakati na malengo yao pamoja na kutoa mwelekeo mpya wa chama.
Ole Sosopi na wenzake watatumikia nafasi hizo kwa muda wa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi kufanyika mwakani 2018. Patrobas Katambi alitangaza kuhamia CCM hivi karibuni kupitia mkutano mkuu wa NEC wa CCM uliofanyika Ikulu jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti wake Rais John Pombe Magufuli

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE