December 3, 2017

NEC YATANGAZA UCHAGUZI MDOGO NCHINI TENATume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid amesema tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika ya kwamba nafasi ziko wazi.

Jimbo la Singida Kaskazini liko kutokana na kujivua uanachama wa CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu, Songea Mjini baada ya kifo cha Leonidas Gama na Longido baada ya Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Onesmo Ole Nangole.

Akizungumzia uchaguzi wa kata sita amesema waziri mwenye na serikali za mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata hizo Tanzania Bara

Alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu(Arusha), Kihesa (Iringa), Bukumbi (Uyui), Kurui (Kisarawe), Keza (Ngara) na Kwagunda (Korogwe).


Amesema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya Desemba 12 hadi 18, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya Desemba 14 hadi 20 mwaka huu

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE