December 18, 2017

NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI ATEMBELEA MKOA WA ARUSHA

 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akishiriki  zoezi la upigaji chapa mifugo  katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
 Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizindua zowezi la upigaji chapa mifugo  katika hifadhi ya Ngorongoro mkoani Arusha.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, (wa kwanza kulia)akizungumza na wananchi  wanoishi katika hifadhi ya Ngorongoro leo baada ya kushuhudia zowezi la upigaji chapa mifugo  mkoa wa Arusha.katikati ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na kushoto, Naibu Muhifadhi Dkt.Maurus  Msuha
 Naibu Muhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,Dkt Maurus  Msuha akishiriki zowezi la upigaji chapa mifungo leo mkoani Arusha.Zowezi la upigaji chapa mifungo likiendelea mkoani Arusha.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG Arusha)

Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na uvuvi Mhe.Abdalla Hamisi Ulega amefanya ziara mkoani Arusha katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kuhamasisha upigaji chapa mifugo.

Akizungumza na baadhi ya wafugaji katika halmashauri ya Ngorongoro Ulega amempongeza mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo, kwa utendaji mzuri wa kazi  hususani katika kuhamasisha upigaji chapa mifugo mkoani humo.

Aidha Mhe Ulega amezijata baadhi ya halmashauri zilizofanya vizuri katika zoezi la upigaji chapa kuwa ni pamoja na Chemba,Kondoa,Maswa,Mafingana Misungwi.

Ambapo mhe. Ulega amewahimiza wafugaji kujitokeza kwa wingi katika zowezi  la upigaji chapa mifungo linaloendelea nchi zima.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE