December 27, 2017

MWANAMKE ASHANGAZWA NA BILI YA UMEME YA DOLA BILIONI 284.

Image result for nishati ya umeme
Bili ya umeme ya zaidi ya dola bilioni 284 ilimshangaza mwanamke mmoja katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani hadi alipogundua kuwa bili hiyo ilikuwa na makosa.
Mary Horomanski kutoka Erie, alisema kuwa bili hiyo ilionyesha kuwa alihitajika kulipa pesa hizo zote ifikapo Novemba mwaka 2018.
Kampuni ya umeme baadaye ilisema kuwa bili sahihi ilikuwa dola 284.46.
Msemaji wa kampuni alisema kuwa hawakufahamu jinsi hitilafu hiyo ilitokea ikionyesha kuwa Bi Horomanski alihitajika kulipa $284,460,000,000 huku akitakiwa kulipa sehemu ya kwanza ya dola 28,176 mwisho wa mwezi huu.
"Sijawi kuona bili ya mabilioni ya pesa,"Alisema  Mark Durbin

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE