December 18, 2017

MUNGU NI ZAIDI YA OIL AU GRIS KWA VYUMA VILIVYOKAZA... TUOMBE


Tunakila sababu ya kukushukuru Mungu kwa fadhili zako kuu na hata kutuwezesha kutamka vema na kuianza tena jumatatu ya Leo maana wewe u mwema. 

Baba Mungu wajua hitaji letu kwako na daima wewe ni Mungu baba yetu na baba siku zote hamwachi mwanae aangamie kuwa nasi safarini, makazini na pia wagonjwa na wote wenye Shida ni wako baba. 

Twakutumaini wewe baba Mungu hivyo hatumtaki kukufundisha nini cha kufanya kwetu na hatuombi twaamini baba hulinda familia yake na mbinu zote za ulinzi wazijua wewe. 

Zaidi sisi wana wako tuzidi kudumu katika upendo, amani huku baba tukitegemea hata viongozi wetu utawapa afya njema 

Sio kwamba baba hutambui kuwa vyuma vimekaza miongoni mwetu wana wako watambua na hatukufundishi jinsi ya kuvilainisha au mbinu ya kuvilainisha iwe kwa Gris oil au maji Baba Twakutumaini wewe

Kwako Mungu baba yetu wa mbinguni twakushukuru daima na wewe ni baba mwema ulindae vema wana wako


AMEN

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE