December 31, 2017

MTU MOJA ATIWA MBARONI URUSI AKIHUSISHWA NA SHAMBULIZI LA ST. PETERSBURG

Image result for shambulizi la St. Petersburg
Mtu mmoja ametiwa mbaroni jana Jumamosi akihusishwa na shambulizi la bomu katika duka moja kubwa mjini St.Petersburg lililojeruhi watu 18.
watu wanane bado wamelazwa hospitali baada ya mripuko kutokea katika eneo la kuhifadhia mabegi ya wateja katika eneo hilo.
Wachunguzi wanasema kifaa kilichotumika katika shambulzi hilo kilichotengenezwa kienyeji kilikuwa na gram 200 za vilipuzi na kingeweza kusababisha madhara makubwa.
Idara ya usalama nchini humo haikumtaja mshukiwa wa shambulizi hilo ama kutoa maelezo zaidi kumhusu.

Kundi la itikadi kali linalojiita Dola la Kiisilamu limedai kuhusika na shambulizi hilo lakini afisa mmoja katika kamati inayohusika na masuala ya usalama katika bunge la nchi hiyo ameonesha mashaka na kusema inawezakana ikawa ni jaribio la kundi la dola la Kiisilamu kutaka kujiongezea umaarufu katika jamii.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE