December 29, 2017

MSUVA AKAMATIKI KWA MWENDO HUU MOROCCO

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya Difaa El Jadidya Morocco Simon Msuva anazidi kuchukua headlines kutokana na kasi na mchango wake anaozidi kuutoa katika club yake ya Difaa El Jadid.
Simon Msuva kwa mara ya pili anafanikiwa kuifungia timu yake goli muhimu katika mchezo wa Ligi Kuu MoroccoMsuva leo ameipatia ushindi wa goli 1-0 timu yake ya Difaa El Jadid dakika ya 52 dhidi ya Hassania Agadir.
Kufunga kwa goli hilo kunamfanya Simon Msuva kusogea katika msimamo wa ufungaji bora kwani goli dhidi ya Agadir limemfanya kutimiza jumla ya magoli 5 na mtu anayeongoza ana magoli saba lakini huu ni mchezo wa pili kwa Msuva kufunga mfululizo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE