December 31, 2017

MKANDARASI GEOFREY MUNGAI ASAIDIA CHAKULA YATIMA VITUO VITATU IRINGA

Mkandarasi Geofrey  Mungai  akimnywesha  uji  mtoto  wa   kituo  cha yatima  Tosamaganga  jana  baada ya  kufikia  kituoni hapo  kutoa  msaada  wa  chakula  cha sikukuu
Mungai  akitoa  msaada  wa  mafuta na  vyakula  kituo cha watoto  yatima  Tosamaganga 
Mtoto  yatima  wa  kituo cha  Tosamaganga  akifurahi  na Mungai
Mungai akiwa  na  watoto  yatima  wa  kituo  cha DBL
MKANDARASI  maarufu  mkoani  Iringa  Geofrey Mungai  ametoa msaada  wa chakula cha  Mwaka  mpya chenye  thamani ya  shilingi  milioni 3 kwa vituo vitatu  vya  yatima  kikiwemo  cha Daily Bread life childreans home (DBL)cha mkimbizi  katika  Manispaa ya  Iringa huku  akimpongeza Rais Dkt  John  Magufuli kwa kuendelea kusaidia yatima Iringa.
 
Akikabidhi msaada   huo  jana kwa  nyakati  tofauti  katika  kituo  cha DBL   ,Lugalo  na  Tosamaganga ,Mungai  alisema kuwa  umekuwa ni  utamaduni  wake na  familia  yake  kutoa chakula na mavazi  kwa yatima siku  za  sikukuu kila mwaka 
 
Mungai  alisema  kuwa  amelazimika  kutoa zawadi  hizo  za  sikukuu  kwa watoto hao  kama njia ya  kuwajali  na kuwafanya  yatima  hao kufurahia  sikukuu  kama  watoto  wenye  wazazi .
 
Hata  hivyo  alitaka  jamii  kuendelea  kuwakumbuka  watoto hao  yatima badala ya  kuendelea kuwatenga na kuwanyanyapaa kwa madai  kuwa watoto hao  yatima hawakupenda  kuwa  yatima ila ni mipango ya Mungu na kuwa  jamii  kuendelea kuwabagua ni kuongeza unyanyapaa kwa watoto hao wasio na hatia mbele  za Mungu.
 
Pia  alisema  kuwa  kupitia kampuni yake  ya ukandarasi  mkoani  Iringa  amekuwa na kawaida ya kutenga bajeti  kwa ajili ya  kuwasaidia  watoto wa kituo  hicho  cha DBL  na vingine mkoani Iringa   na kuwa ataendelea  kufanya  hivyo kwa  kuwaweka  jirani  zaidi  watoto hayo kama  sehemu ya familia  yake.
 
Aidha  Mungai  alipongeza  jitihada  kubwa   zinazofanywa na uongozi  wa  kituo  hicho katika kuwalea  yatima hao na  kuwa  mbali ya  kuwepo kwa vituo  vingi  vya  yatima  ila kituo  hicho kimekuwa  kikiwalea yatima  hao  kama familia na kuwa ni vigumu  kuweza kuamini kama watoto hao ni yatima  kutokana na maisha  wanayoishi  kituoni  hapo.

Alisema  jitihada  mbali mbali  zimekuwa zikifanywa na vionngozi wa  serikali akiwemo Rais Dkt  Magufuli kuona  jamii yenye matatizo wakiwemo  yatima  hao  wanapata zawadi mbali mbali kipindi  cha  sikukuu.

Hivyo  aliiomba  jamii kuiga mafano wa Rais katika  kuwajali  watoto  yatima  kwa   kuwakumbuka wakati wa  sikukuu mbali  mbali .
 
  mkurugenzi  mtendaji  wa  kituo  hicho mchungaji Mpeli Mwaisumbe mbali ya kumpongeza Geofrey Mungai na familia  yake  kwa kutoa msaada  huo   pia  alisema  kuwa Mungai amekuwa bega kwa  bega  na  kituo  hicho .

Mchungaji Mwaisumbe  aliwataka   viongozi wa dini  kufanya kai ya  kuliombea  Taifa  pamoja na  Rais Dkt Magufuli  kwa  kazi  kubwa na nzuri  anayoifanya  badala ya  viongozi wa  dini  kutumia  nyumba za  ibada kuishambulia   serikali .

Mkurugenzi  wa kituo hicho Mchungaji  Neema Mpeli  akishukuru  kwa  msaada  huo  alisema  kuwa jitihada  zinazofanywa na  mkandarasi  Mungi  katika  kuwakumbuka   watoto  hao  ni kubwa  na  kuwa amekuwa kiunganishi kati ya  watoto  hao  na familia  yake .

 
 
 

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE