December 26, 2017

MISRI YAWANYONGA WATU 15 KWA MAUAJI YA WANAJESHI TISA

Image result for wanajeshi Misri
Misri leo imewanyonga watu 15 waliotiwa hatiani kwa mauaji ya wanajeshi tisa mwaka 2013 katika jimbo la Sinai kaskazini mwa nchi hiyo.

 Mahakama ya kijeshi iliyokuwa ikisikiliza mashitaka dhidi ya walalamikaji ilitupilia mbali rufaa yao na kuunga mkono hukumu ya awali. 

Watu hao walitiwa hatiani kwa kuhusika na mauaji ya Sajenti mmoja wa jeshi na wanajeshi wengine saba katika rasi ya Sinai miaka minne iliyopita. 

Misri imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi yanayofanywa na makundi ya itikadi kali mengi yakivilenga vikosi vya usalama na jamii ya wakristo wachache tangu mapinduzi yaliyofanywa na jeshi kumuondoa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi mwaka 2013. 

Novemba mwaka huu zaidi ya waumini 300 waliuawa katika msikiti mmoja kaskazini mwa Sinai likiwa ni shambulizi baya zaidi la hivi karibuni katika historia ya nchi hiyo.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE