December 31, 2017

MHAKAMA MISRI YAMTIA HATIANI RAIS WAZAMANI MORSI KWA KOSA LA UCHOCHEZI

Image result for RAIS WA ZAMANI MORSI
Mahakama moja nchini Misri jana Jumamosi imemtia hatiani rais wazamani wa Misri Mohammed Morsi na watu wengine 19 kwa kosa la kuikashifu mahakama.
Kutokana na kosa hilo mahakama imewahukumu kwenda jela miaka mitatu katika hukumu hiyo iliyotangazwa moja kwa moja kupitia Televisheni.
Kesi hiyo ilikuwa ikiwahusisha washitakiwa 25 ambapo watano miongoni mwao ikiwa ni pamoja na mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Alaa Abdel- Fattah na mchambuzi wa masuala ya kisiasa Amr Hamzawy walitozwa faini ya paundi za Misri 30,000 kila mmoja.
Abdel-Fattah anatumikia kifungo cha miaka mitano kwa kushiriki maandamano ambayo hayakuwa na kibali kisheria mwaka 2013.

 Washitakiwa wote wanadaiwa kuikashifu mahakama kwa kutoa kauli ambazo zilitangazwa ama kupitia Televisheni, radio, mitandao ya kijamiii au katika machapisho ambayo mahakama imeona ni uchochezi.

0 comments:

Post a Comment

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0754 026299 Email . fgodwin94@gmail.com , ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE